Moja ya Ahadi za Rais Magufuli alipokuwa kwenye majukwaa mbalimbali ya kampeni ni kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za afya, na jambo hilo limekuwa likifanywa na watendaji mbalimbali alio wateua kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Ambapo siku ya leo Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amekabidhi daipa elfu 85,000 kutoka Taasisi ya GSM Foundation katika Hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam, ambapo ameeleza kuwa Daipa hizo zitagawiwa katika vituo vya afya 26 vya wilaya yake ambapo wazazi wenye watoto wanaohudhuria kliniki na wale watakaojifungua hivi karibuni watakabidhiwa.
Aidha Mkuu wa wilaya huyo ameongeza kuwa serikali itaendelea kuboresha Huduma za Afya, na kupongeza jitihada zinazofanywa na GSM Foundation huku akiwataka wadau wengine waige mfano huo, na kuwaomba GSM Foundation waendelee kuwasaidia kwani yapo masuala mbalimbali ya kiafya yanayohitaji msaada wao.
No comments:
Post a Comment