Monday, September 5, 2016

TAARIFA MPYA KUTOKA CUF MCHANA HUU

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgpvC2ANFXkOYMfRUkNVnexxmNzZP3DjAoYWvU7Vs8oPebhBdTOwOcADeHDsKujeD6ay0UyWAnJ16OpnMLQXLN0h5k173s_njm6HVojEm23Nxs9UN-x370hA6GA6UB83Eerbygt44yNe5o/s640/SAM_5072.JPGTAARIFA ZA UPOTOSHWAJI ZINAZOTOLEWA NA BAADHI YA WANACHAMA WALIOPELEKEA MALALAMIKO YAO KWA MSAJILI
WA VYAMA VYA SIASA NCHINI



KUMEKUWA NA taarifa za upotoshwaji zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii na vilevile viongozi wa kitaifa wamekuwa wakipigiwa simu na au kupokea ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa wanachama, marafiki na wapenzi wa CUF wakijulishwa kuwa baadhi ya wanachama waliopeleka malalamiko yao kwa msajili wa vyama vya siasa kuomba kuingilia kati madai yao ya kutaka kumrejesha aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Taifa Mheshimiwa Prof. Ibrahim Lipumba ambaye tarehe 5 mwezi August, mwaka 2015 alifanya maamuzi magumu ya kujiuzuru nafasi hiyo kwa ridhaa yake bila kushurutishwa mbali ya kunasihiwa sana asichukue maamuzi hayo na viongozi mbalimbali wa chama, viongozi wa dini, marafiki na wapenzi wa CUF na wanachama kwa ujumla.

Ujumbe huo wa upotoshaji unasema na nanukuru;
“Atimaye leo msajili wa vyama vya siasa atinga makao makuu ya CUF kuweka zuio kwa ........Sefu asifanye shughuli zozote za chama napia asiingie hapo ofisini adikesi ya msingi itakapo sikilizwa hakiiiiiiiii” Mwisho wa kunukuru.

Wanachama hao ambao wanajitambulisha kwa jina la ‘wafia chama’ au ‘MUNGIKI TEAM’ wamekua wanaionyesha barua hiyo iliyotoka kwa msajili kwa vyombo vya habari na kuisoma kwa kupotosha ili kufikia adhima yao ovu dhidi ya chama. Pia wanaendelea na kusambaza taarifa eti leo Jumatatu tarehe 5/9/2016 kuna mabomu ya machozi yamepigwa ofisi kuu buguruni kuwatawanya viongozi waliokuwa wanataka kuingia ofisini kuendelea na shughuli zao.

Napenda kuchukua fursa hii kuwajulisha kuwa taarifa hizo si sahihi hata kidogo, hazina ukweli. Tumefanya mawasiliano na Msajili wa vyama vya siasa kujua kama kuna barua nyingine aliyoitoa zaidi ya ile ya tarehe 2/9/2016 ambayo pia walalamikaji wamepewa nakala yao amekanusha taarifa hizo na yote wanayoyaeleza juu yake. Rejea barua hiyo hapa chini.

Shughuli za kiofisi za chama cha CUF zinaendelea kama kawaida na katibu mkuu wetu Maalim Seif Sharif Hamad na watendaji wengine wakimemo wakurugenzi/manaibu wakurugenzi wameendelea na majukumu yao ya kikazi kama kawaida. Rejea picha za baadhi ya watendaji na za Katibu Mkuu akiwa ofisini leo Buguruni.

Tunawaomba wanachama wetu, marafiki wa CUF, wapenzi wa chama chetu na watanzania kwa ujumla kuondoa hofu juu ya propaganda hizi zinazofanywa na wasio na nia njema na chama cha CUF na NGUVU YA USHINDANI WA KWELI WA KISIASA HAPA NCHINI ambao wanashirikiana na washindani wetu wakuu wa kisiasa CCM kutaka kutuyumbisha na kuwayumbisha watanzania wapenda mabadiliko. CUF inaamini kuwa muda si mrefu mtawajua dhamira zao na watajipambanua uhalisi wao (true color) na watakwenda watakakokwenda. Chama cha CUF ni taasisi kubwa ya kisiasa nchini yenye viongozi makini, welevu na weledi wa kushughulikia masuala ya kisiasa, kiutawala na kiuongozi. 

CUF itaendelea kuwa IMARA ZAIDI, NGANGARI ZAIDI.
Aidha, THE CIVIC UNITED FORNT (CUF-Chama Cha wananchi) kinawaomba wahariri wa vyombo vya habari na waandishi kwa ujumla pindi wanapohitaji kupata taarifa za chama wasisite kufanya mawasiliano na KURUGENZI YA HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMAH inayoongozwa na Mkurugenzi wake Mhe. Salimu Bimani – 0777 414112/ 0752 325227 na au K/Naibu wake – Mbarala Maharagande- 0784 001408/ 0621 715795.

Pia kwa kupata taarifa za chama munaweza kufanya mawasiliano na viongozi wengine wafuatao;
Mhe. Julius Mtatiro –
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongizi Taifa – 0787 536759/ 0717 536759
Mhe. Joran Bashange-
K/Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara -0784 941 774 / 0777 941774
Mhe. Nassor Mazrui –
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar -0777 426975
Mhe. Shaweji Mketo –
Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni, Mipango Na Uchaguzi – 0782 082080
HAKI SAWA KWA WOTE
Mbarala Maharagande
K/Naibu Mkurugenzi Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
maharagande@gmail.com

No comments: