Saturday, September 10, 2016

TETEMEKO LA ARDHI LALETA MAAFA MAKUBWA BUKOBA MKOANI KAGERA

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera zinasema kuwa kuna tetememko la ardhi limetokea na kusababisha madhara makubwa.
Mkuu wa wilaya ya Bukoba Mh. Deodatus Kinawiro akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu amesema tetemeko lililotokea mchana leo lilikuwa ni kubwa na limeathiri majengo mengi na kusababisha majeruhi na vifo hata hivyo bado vikosi vya uokoaji pamoja na majeshi la ulinzi na usalama vinaendelea kuokoa majeruhi wa ajali hiyo ya Tetemeko la ardhi.
DC Kinawiro ameongeza kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye baada ya kufanya kazi ya uokoaji na tathmini ya athari ya tetemeko hilo.

4





No comments: