Sunday, September 11, 2016

Waziri Moldiline Castico Azinduzi wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja.


Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati Unguja Mhe. Simai Mohammed Said, akizungumza na Vijana wa Kisiwa cha Uzi wakati wa uzinduzi wa Baraza la Vijana la Shehia hiyo lililozinduliwa na Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Moldiline Castico katika viwanja vya Skuli ya Uzi.  
Mc wa Mkutano huo wa Uzinduzi wa Baraza la Vijana wa Shehia ya Kisiwa cha Uzi akisoma ratiba ya Uzinduzi huo katika viwanja vya Skuli ya Uzi Wilaya ya Kati Unguja.
Mwanachama wa Baraza la Vijana la Shehia ya Kisiwa cha Uzi Unguja Khadija Said akisoma Quran Tukufu kabla ya Uzinduzi wa Baraza lao la Vijana la Shehia ya Uzi lililozinduliwa na Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe, Moldiline Castico.
Vijana wa Baraza la Vijana la Shehia ya Kisiwa cha Uzi wakicheza maigizo ya kuhamasisha Vijana kujiunga na Mabaraza ya Vijana kwa Maendeleo yao katika kujikwamua Kiuchumi.  
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu akiwa na Viongozi wa meza kuu wakifuatilia mchezo wa maigizo unaohamasisha Vijana kujiunga na Mabaraza la Vijana katika Shehia zao.,
Mwanachama wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha  Uzi Salma Tunda akisoma risala yao mbele ya Mgeni rasmin wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya skuli ya uzi. 
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi Farashuu Mussa akitowa salamu za Baraza lake kwa mgeni rasmin wakati wa uzinduzi huo.
Sheha wa Shehia ya Kisiwa cha Uzi Hamad Ramadhani akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa Baraza la Vijana wa Kisiwa cha Uzi
Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Mhe Mashavu Sukwa akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi Unguja na kuwataka Vijana kutumia Mabaraza la Vijana kwa maendeleo yao katika kujitafutia Ajira. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Wilaya yac Kati Unguja Mhe Simai Mohammed Said akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Baraza la Vijana la Shehia ya Kisiwa cha Uzi na kuichangia shilingi laki mbili kwa kukuza mtaji wa Baraza hilo katika miradi yao endelevu.  
Waziri Moldiline Castico na viongozi wa meza kuu wakimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu akitowa salamu za Mbunge wa wake kwa Vijana wa Shehia ya Kisiwa cha Uzi wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Uzi.
Waziri Moldiline Castico akimkabidhi fedha Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi Farashuu Mussa fedha zilizotolewa mchango na Mwakilishi wa Jimbo la hilo Mhe Simai Mohammed Said ikiwa ni mchango wake kwa Baraza hilo la Vijana wa Shehia ya Uzi.

Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Moldiline Castico akiwahutubia Vijana wa Baraza la Shehia ya Kisiwa cha Uzi wakati wa kulizindua Baraza hilo na kuwaasa Vijana kubuni miradi ya Maendeleo yatakayowaletea Tija katika kukuza Uchumi wao kupitia Mabaraza hayo. uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Skuli ya Uzi.Wilaya ya Kati Unguja Jimbo la Tunguu Zanzibar.
Vijana wa Baraza la Vijana Shehia ya Kisiwa cha Uzi wakimsikiliza Mgeni rasmin wakati wa uzinduzi wa baraza lao lililozinduliwa na Waziri wa Kazi Vijana Uwezeshaji Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Moldiline Castico.

Sheha wa Shehia ya Uzi Ngambwa Amour Ali akisoma dua baada ya hafla ya uzinduzi wa Baraza la Vijana la Shehia ya Kisiwa cha Uzi, uliofanyika katika viwanja vya skuli ya Uzi Wilaya ya Kati Unguja Jimbo la Tunguu Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot
Zanzinews.com.  

No comments: