Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mkunguakihendo wakati wa ziara ya kikazi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Rustika Turuka akisisitiza jambo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Kuzungumza na baadhi ya viongozi wa Vitongoji, Kata na Vijiji katika ukumbi wa shule ya sekondari Mkunguakihendo wakati wa ziara ya kikazi
Wananchi wakisikiliza kwa makini maagizo ya serikali kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua jinsi ujenzi wa maabara unavyosuasua katika shule ya sekondari Mkunguakihendo ambapo amemuagiza Diwani kusimamia ujenzi huo uli kufikia mwakani maabara ianze kutumika
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua utengenezaji wa Chumvi katika Mbuga ya Mwakilongo iliyopo Kijiji cha Itagata, Kata ya Kikio
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, akiwakwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Wakuu wa Idara na Vitengo, Diwani wa kata ya Kikio Steven Sinda, Walimu na Viongozi wa ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Kata ya Mkunguakihendo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua ujenzi wa shule ya Awali na Msingi Simbikwa
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Misughaa Kata ya Misughaa
Baadhi ya viongozi mbalimbali wakiwemo walimu walioalikwa kwenye kikao cha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Mkunguakihendo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akitafsiri kwa vitendo ilani ya Chama Cha Mapinduzi iliyoshinda uchaguzi uliofanyika Octoba 25, 2015
Baadhi ya wakazi wa kijiji Cha Misughaa Kata ya Misoghaa wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo
Dc Mtaturu akizungumza na wajasiriamali wanazalisha Chumvi katika Mbuga ya Mwakilongo iliyopo katika Kijiji cha Itagata, Kata ya Kikio ambapo amemtaka Afisa Ustawi wa jamii kuhakikisha vikundi vinasajiliwa kwa ajili ya kuwa na uzalishaji mkubwa zaidi na wenye tija
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari Dkt Shein iliyopo Kata ya Misughaa ambapo pamoja na kupatikana jumla ya shilingi milioni saba kwa ajili ya ujenzi wa maabara hiyo lakini bado hata msingi haujakamila, hivyo agizo limetolewa kwa kufanyika uchunguzi wa namna zilivyotumika fedha hizo
Wananchi wa Kijiji cha Misughaa wakisikiliza kwa makini maagizo ya serikali kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa ziara ya kukagua shughuli za maendeleo
Na Mathias Canal, Singida
Wananchi wametakiwa kuachana na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya
wanasiasa kwa kuwataka kutochangia shughuli za maendeleo ikiwemo
kuchangia ujenzi wa maabara kwani kufanya hivyo ni kuwapumbaza wananchi
ilihali wanasiasa hao wanaofanya hivyo wamesoma na kufikia kuwa na
nafasi nzuri kwenye serikali ambapo pia watoto wao wana elimu nzuri na
wengine wanasoma nje ya nchi.
Mwito huo umetolewa na Mkuu wa
Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika ziara yake ya kikazi
iliyoanza leo katika Kata mbili za Kikio na Kata ya Misughaa.
Dc Mtaturu amewataka viongozi hao kutoyakimbia maeneo yao ya kazi
ikiwemo majimbo na kuachana na uongozi wa sifa zisizokuwa na tija badala
yake wanapaswa kurejea Katika maeneo yao ya utendaji ili kushiriki kwa
pamoja na wananchi katika shughuli za Maendeleo.
Mraturu ambaye
ameanza ziara hiyo ikiwa na engo la kutembelea miradi ya maendeleo na
kujua maeneo yote anayofanyia kazi, Kuhimiza shughuli za Maendeleo na
kuwakumbusha wanasiasa kuwa uchaguzi mkuu ulifanyika Octoba 25 Mwaka
jana na kumalizika hivyo wakati huu ni wa kufanya kazi na kuzikabili
changamoto zinazowatatiza watanzania kwa miaka mingi.
Amesema
kuwa serikali inaposema wananchi wachangie shughuli za maendeleo haina
maana kwamba wananchi wachangie pesa pekee bali wanaweza kuchangia
mchanga, Tofali na nguvu zao katika kuhakikisha Vitongoji na Vijiji vyao
vina imarika katika miradi mbalimbali yenye tija katika jamii.
Dc Mtaturu amewataka wanasiasa kutojificha kwenye kichaka cha Demokrasia
huku hawana nidhamu badala yake kuihubiri demokrasia kwa kufanya
shughuli za kuwawezesha wananchi kuimarika katika shughuli mbalimbali
zitakazo wawezesha kuondokana na umasikini uliokithiri nchini Tanzania.
Ameahidi kuwavalia njuga baadhi ya wataalamu wote walioajiriwa na
serikali kwa ajili ya kuwatumikia wananchi lakini wamebadili muelekeo na
kuanza kufanya shughuli za siasa badala ya kuzitendea haki taaluma zao
katika kuyafikia matokeo makubwa ya kipato cha wananchi.
"Watumishi wote wa serikali, Wakuu wa idara na vitengo pamoja na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya wanapaswa kufanya kazi moja tu ya
kutafsiri kwa vitendo ilani iliyoshika hatamu ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM)" Alisema Mtaturu
Sambamba na hayo pia amewasihi wananchi
kutokata miti ovyo kwani jambo hilo litapelekea kukosekana kwa mvua za
kutosha na kusababisha mabadiliko ya tabia nchi badala yake wanapaswa
kupanda miti zaidi katika maeneo yao ya makazi na maeneo ya mashamba.
Dc Mtaturu ameahidi kushirikiana na viongozi wote waliochaguliwa katika
uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ili kuchochea shughuli
za maendeleo na sio kushughulika na viongozi wa vyama kwani muda wa
kuhangaika na vyama ni wakati wa kampeni zingine kwa ajili ya uchaguzi.
Dc Mtaturu kabla ya kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara
ametembelea na kujionea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa
maabara katika shule ya Sekondari Mkunguakihendo na Shule ya Sekondari
Misughaa.
Amesema kuwa ni jambo la aibu kwa baadhi ya wanasiasa
ambao wamegeuka kuwa matapeli wa hoja kwa kuwahadaa wananchi na kupotea
katika maeneo yao ya kazi lakini huibuka tena wakati wa kampeni.
Kwa upande wa wananchi waliopata wasaa
wa kuuliza maswali wamemtaka mkuu huyo wa Wilaya kuwasaidia katika
kuimarisha uchumi na shughuli za maendeleo ya wananchi kwani Wilaya ya
Ikungi imedumaa kimtazamo wa maendeleo tangu mwaka 2011 mpaka sasa.
Katika sekta ya Kilimo Dc Mtaturu ameitaja Pamba inayozalishwa Wilayani Ikungi kuwa ni ya kiwango cha ubora wa hali ya juu (Grade One) kitaifa hivyo amewataka wananchi hao kuongeza zaidi uzalishaji ili kuongeza ufanisi wa kipato cha mtu mmoja mmoja na kukuza uchumi wa Taifa kupitia zao hilo la biashara.
Dc Mtaturu amesema kuwa kwa mujibu wa kampuni inayosimamia kilimo hicho ya BioSuston imeeleza kuwa msimu uliopita ulikuwa na mafanikio makubwa kwa wakulima wa pamba Wilayani Ikungi ambapo hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amemuagiza Mkurugenzi kumpeleka Afisa Kilimo awasaidie zaidi kuwapa mbinu bora za kilimo ili kuimarisha kilimo hicho na kupata mazao mengi yenye tija.
Katika hatua
nyingine Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ameagiza
kuhamishwa kituo cha kazi mganga Mkuu wa Zahanati ya Misughaa Steven
Kirita aliyafanya kazi kwa zaidi ya miaka 20 katika kituo hicho huku
akihusishwa na tuhuma za ulevi uliokithiri.
No comments:
Post a Comment