Meneja wa Huduma za kijamii wa Tigo Woinde Shisael akizngumza na wanahabari wakati wa Uzindizi wa shindano hilo leo Jijini Dar es salaam |
Kampuni ya simu ya Tigo
kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Reach For change wamezindua
shindano la Tuzo ya mwaka ya kidigitali ya Tigo Change Makers,shindano
linalolenga kuwatambua na kuwasaidia wajasiriamali jamii kwa kutumia zana za
kidigitali na Technologia katika kuboresha Jamii pamoja na matokeo yake kwa
Vizazi vya Baadae,ambapo kwa mwaka huu Tigo inaangalia ubunifu uliojikita
katika mtazamo wa elimu kupanua kujumuisha kidigitali na ambao unalenga kusaidia
shiughuli za Ujasiriamali.
Faraja Nyarandu Pichani alishinda dola 20,000/- Mwaka 2014 katika shindano la @TigoTanzania #DigitalChangemakers.leo akizungumza mafanikio aliyoyapata baada ya ushindi na kuwezeshwa na Tigo Tanzania |
Jumla ya fedha taslim
dola za marekani 20,000 zitatolewa kwa kila wazo litakaloshinda kati ya mawazo
mawili yatakayoshinda na hivyo kutoa nafasi ya kuingia katika malezi ya Reach For
change,mafunzo ya kibiashara na mtandao wa dunia wa wajasiriamali wengine wa
kijamii.ambapo kipindi cha kutuma maombi kwa ajili ya kushiriki katika shindano
hilo kimefunguliwa Rasmi leo hadi November 21,2016.
Akiangumza katika
mkutano wa wanahabari wakati wa uzinduzi huo Meneja wa Huduma za kijamii wa
Tigo Woinde Shisael amesema kuwa Tigo inayo furaha kuendesha Tuzo ya kidigitali
ya Tigo change makers mwaka huu ikiwa na mtazamo Mpya,huku akisema kuwa Timu ya
tigo ina hamu sana ya kusaidia Ubunifu wa Kidigitali na shughuli za
ujasiriamali nchini Tanzania.
Shisael ameongeza kuwa
Tuzo ya kidigitali ya Tigo Changemakers ni niia kubwa ya kuwasaidia wabunifu
kijamii wazuri walio na weledi ambao wanahitajika nchini katika kuwawezesha
kubadilisha maisha ya jamii kupitia masuluhisho ya Kidigitali.
Ikiwa ni mwaka wa Tano
ambapo Tigo Reach For change wanaendesha shindano hilo la kutafuta mjasiriamali
jamii,Bi Woinde amepongeza kazi za washindi waliotangulia na kuhimiza wengine
kushirikiana nao katika mawazo yao.
“Hivi sasa tutawasaidia
wajasiriamali 9 kupitia mkakati wa kidigitali wa Tigo Changemakers.wametumia
vizuri fedha walizopewa,mafunzo ushauri,na Zaidi ya yote kuleta mabadiliko
nchini Tanzania”amesema Meneja huyo wa Huduma za kijamii Tigo.
Carolyne Ekyarisiima Mshindi wa mwaka 2015 akieleza machache mbele ya wanahabari |
Akitaja mifano ya
washindi ambao wamenufaika na shindano hilo tangu lianzishwe amesema kuwa Carolyne Ekyarisiima ni mmoja
washndi wa tuzo ya Tigo Change makers ambaye amekua akifanya kazi ya kuziba
pengo la kijinsia katika Technologia ya Habari na mawasiliano kupitia
ujasiriamali kijamii wa Vifaa na watoto wa kike(Apps &girls)
“Mwaka 2015 Carolyne
alileta mabadiliko kwa wasichana 1000,kupitia mfumo wa klabu mashuleni, warsha,maonesho,mawasiliano
ya simu,kambi za mijadala na mashindano”amesema Shisael na kuongeza kuwa “sio
tu kwamba mkakati huu unasaidia kuhakikisha watoto wengi wa kike kuzifikia
Teknolojia za kidigitali,hali kadhalika inawezesha kuwa Viongozi wa baadae wa
Teknolijia Ya habari na mawasiliano.
Carolyne ni mmoja wa
mfano wa wabunifu weledi wa kidigitali ambao Tigo inawatafuta ili iwasaidie
kupitia tuzo ya mwaka huu,Shisael amesema anatarajia kupitia Upya ubunifu wa
kidigitali wa kuvutia ambao utawasilishwa katika shindano la mwaka huu.
No comments:
Post a Comment