Mauzo ya Soko
Idadi ya mauzo imeongezeka
kwa asilimia 39% na kufikia TZS 5.3 Bilioni kutoka TZS 3.8 Bilioni wiki
iliyopita.
Idadi ya hisa zilizouzwa
na kununuliwa imeshuka kwa asilimia 91% hadi 869,453 kutoka 9.8 Milioni wiki
iliyopita.
Kampuni tatu
zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni zifwatazo:
1.
CRDB kwa asilimia 51.8%
2.
TBL kwa asilimia 44.44%
3.
DCB kwa asilimia 1.22%
Ukubwa wa Mtaji wa Soko
Ukubwa wa mtaji wa soko umepanda
kwa asilimia 1% na kufika Trilioni 21.8 kutoka Trilioni 21.6 wiki iliyopita.
Ukubwa wa mtaji wa
makampuni ya ndani pia umepanda kwa asilimia 0.4% hadi Trilioni 8.19 kutoka
Trilioni 8.16 wiki iliyopita.
Viashiria (Indexes)
Sekta ya viwanda
imejitokeza wiki hii kuongezeka Zaidi ya pointi 26 baada ya bei ya hisa za
TBL kuongezeka kwa asilimia 0.76%:
Bei za hisa za makampuni
mengine ya ndani ziliendelea kubaki kwenye kiwango kile kile na kupelekea
viashiria vya sekta za huduma za kibenki na za kibiashara kubakia kwenye
kiwango kile kile wiki hadi wiki.
. by Exaud Msaka Habari on Scribd
No comments:
Post a Comment