Baadhi ya wakulima wa zao la korosho waliohudhuria mnada wa wazi
uliofanyika leo katika ghala la Denyecha halmashauri ya mji Nanyamba
wilayani Mtwara.(Picha na Haika Kimaro) |
Na Mwandishi wetu,Habari24 Blog
Wakulima wa zao la korosho mkoani Mtwara leo wameendelea kushirikishwa katika mnada wa wazi na
kupata fursa ya kuchagua bei juu kuliko zote jambo ambalo halikuwa
likifanyika hapo awali.
Wakizungumza na Mtandao huu wakulima waliohudhuria mnada wa
nne uliofanyika katika halmashauri ya mji Nanyamba wilaya ya Mtwata
walisema kitendo cha minada kuwa wazi kitawawezesha kuboresha maisha yao
ambapo kilo moja ya korosho ghafi imeuzwa kati ya Sh 3,762 hadi 3,805
ambapo ni sawa na tani 5,933 zimeuzwa.
Akizungumza mkulima Alhaji Mohamed alisema korosho kuwa na bei nzuri kutawasaidia kuinua uchumi wao na kuboresha maisha.
"Zamani tulikuwa hatushirikishwi kwenye mnada lakini sasa
hivi tunakuwashirikishwa na bei imekuwa nzuri tunapata matumaini ya
kuboresha maisha yetu kwasababu haijawahi tokea tangu nizaliwe,"alisema
Mohamed
Naye Zuhura Hamis aliiomba serikali kuhakikisha wanawajengea viwanda vya kubangua korosho ili kuongeza ajira kwa vijana.
"Sasa bei ni nzuri kwasababu wakulima wenyewe
tunashirikishwa moja kwa moja lakini tunaiomba serikali itujengee
viwanda vya kubangua korosho zetu zikiwa hapa nyumbani ili kuongeza
ajira pia, "alisema Hamis
Akizungumza Mbunge wa jimbo la Ndanda,Cecil Mwambe
aliwataka wakulima kuvumilia wakati wakisubiri malipo yao badala ya
kuuza korosho nje ya mfumo na kuibiwa.
Aidha aliwataka waendelee kushiriki katika minada kuona
yanayofanyika ili kuondokana na malalamiko yaliyokuwa yakitokea siku za
nyuma.
Wakulima niendelee kuwasihi sana kuuza korosho zenu kwa
mfumo wa stakabadhi ghalani msikubali kurubuniwa na watu wanaonunu
kangomba kwasababu watakupa Sh 1,500 kwa kilo lakini pia kipimo chake
sio halisi na yale malalamiko ya kupanga bei hayatakuwepo, "alisema
Mwambe
No comments:
Post a Comment