Wakati
serikali ya Tanzania ikitangaza
kuwa na ugeni mkubwa kesho jumapili ambapo mfalme wa Moroco Mohamed VII ambaye
kwa mujibu wizara ya mambo ya nje mfalme huyo atafanya ziara nchini,hatimaye
Vijana wa Tanzania kupitia
kamati ya mshikamano kati ya Tanzania
na watu wa sahara magharibi TANZANIA SAHRAWI SOLIDARITY COMMITTEE-TASSC
wameanza kutoa ujumbe mbalimbali kwa mfalme huyo.
Ikimbukwe
kuwa kwa miongo minne sasa moroko imekuwa ikiikalia kimabavu nchi ya sahara
magharibi kinyume na sheria na taratibu za kiamataifa jambo ambalo limewafanya
vijana hao kuamua kuamka na kufikisha ujumbe kwa mfalme huyo wa morocco kuwa
swala hilo sio
sahihi.
|
Mratibu wa mawasiliano kwa umma wa
kamati hiyo ya TASSC Bwana Noel c Shao katikati akizngumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam Kuhusu Ziara hiyo ya mfalme wa Moroko |
Akizungumza
na wahabari mapema leo Jijini dar es salaam mratibu wa mawasiliano kwa umma wa
kamati hiyo ya TASSC Bwana Noel c Shao ametaja mambo kadhaa ambayo vijana hao
wametoa kama ujumbe kwa mfalme huyo wa morocco kuwa ni kama yafuatayo ---------
1-Tumesikitishwa
sana na kitendo cha moroko kuendelea kuikalia kimabavu nchi ya sahara magharibi
licha ya uamuzi wa kihistoria uliotolewana na mahakama ya kiamataifa ya haki ICJ kwenye hukumu yake ya mwaka 1975 kwamba
kinyume na madai ya moroko hakuna mahusiano yoyote yale ya kihistoria au ya
kisheria baina ya sahara Magharibi na Moroko yanayoweza kuinyima sahara
Magharibi Kujitawala yenyewe.
2-Tumesikitishwa
sana na kitendo cha moroko kuendelea kupuuzia wito wa umoja wa Africa,umoja wa
mataifa,na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla wake na kuipatia sahara magharibi
haki yake ya kujitawala,Tunapinga vikali mbinu za moroko kuendeleZa hila
mbalimbali ili kuzuia ujumbe wa umoja wa mataifa wa kura ya maoni nchini sahara
Magharibi (The united Mission for Referundum in Western sahara MINURSO) tangu
ulipounda mwaka 1991.
3
Tunamtaka mfalme wa morocco kuwaacha huru wafungwa wote wa kisiasa na
wanaharakati wanaoshikiliwa kwenye magereza mbalimbali kwenye maeneo ya sahara
magharibi yanayokaliwa kimabavu na Moroko.
4Tunamtaka mfalme wa Moroko kuacha mara moja kunyonya
Rasilimali za wasahrawi hasa madini na Phosphate na rasilimali bahari kwenye
maeneo inayoyakalia kimabavu.
5-Tunamtaka
mfalme wa Moroko kuacha mara moja vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu
kwenye maeneo inayoyakali kimabavu kama vile kuwakamata wanaharakati,wa
kisahrawi kuwaweka kizuizini,kuwazuia waangalizi wa kimataifa,waandishi wa
habari na wajumbe wa jumuiya mbalimbali za kimataifa kuingia katika maeneo ya
wasahrawi yanayokaliwa kimabavu na moroko.
6-Tunamtaka
mfalme wa moroko kuacha mara moja vitendo vya kibeberu vya kuikalia sahara
Magharibi. Ni aibu kwa nchi moja ya kiafrika wala nchi nyingine ni wakati
muafaka sasa kwa sahara Magharibi Kupewa Uhuru wake.
Aidha
baada ya maombi ya vijana hao kwa kiongozi huyo wa Moroko wameitaka serikali ya
Tanzania
kutoyumba kimsimamo kuhusu swala la Sahara Magharibi na kamwe Diplomasia ya
uchumi isiwe kisingizio cha kuizika Misingi Yetu ya uhuru ,Utu,Undugu,na
kuwapigania wanyonge.
|
TAMKO LA KAMATI YA MSHIKAMANO WA TANZANIA NA SAHARA
MAGHARIBI (TANZANIA SAHRAWI SOLIDARITY COMMITTEE) KUHUSU ZIARA YA MFALME
WA MOROKO NCHINI TANZANIA
UTANGULIZI
Taarifa rasmi iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki inaonyesha kuwa Mfalme wa Moroko Mohamed VI atafanya
ziara nchini Tanzania kuanzia tarehe 23 hadi 25 Oktoba 2016.
Kwa kupitia ziara hii, sisi vijana wa Tanzania kupitia Kamati yetu ya
Mshikamano Kati ya Tanzania na Watu wa Sahara Magharibi (Tanzania
Sahrawi Solidarity Committee-TASSC) tunapenda kufikisha ujumbe mahsusi
kwa Mfalme wa Moroko, Watu wa Sahara Magharibi, Serikali ya Tanzania na
Jumuiya ya Kimataifa.
Ikumbukwe kuwa kwa zaidi ya miongo minne, Moroko imekuwa ikiikalia
kimabavu nchi ya Sahara Magharibi kinyume na sheria na taratibu za
kimataifa. Sisi kama vijana wa Afrika ambao tunajali misingi ya utu,
umoja na mshikamano wa Afrika kamwe hatuwezi kulinyamazia suala hili na
kuisaliti ndoto ya waasisi wa Umoja wa Afrika waliosisitiza kuwa “Afrika
haiwezi kuwa huru hadi pale nchi zote za kiafrika zitapokuwa huru”
UJUMBE KWA MFALME WA MOROKO
1. Tumesikitishwa sana na kitendo cha Moroko kuendelea kuikalia kimabavu
nchi ya Sahara Magharibi licha ya uamuzi wa kihistoria uliotolewa na
Mahakama ya Kimataifa ya Haki (International Court of Justice-ICJ)
kwenye hukumu yake ya mwaka 1975 kwamba, kinyume na madai ya Moroko,
hakuna mahusiano yoyote yale ya kihistoria au ya kisheria baina ya
Sahara Magharibi na Moroko yanayoweza kuinyima Sahara Magharibi haki
yake ya kujitawala yenyewe
2. Tunalaani vikali mbinu za Moroko kuendelea kuikalia kimabavu kwa
zaidi ya miaka 40 nchi ya Sahara Magharibi na kufumbia macho wito wa
Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wa kuipatia uhuru wake nchi ya
Sahara Magharibi. Tunapinga vikali njama na hila za Moroko kuzuia Ujumbe
wa Umoja wa Mataifa wa Kura ya Maoni Nchini Sahara Magharibi (The
United Nations Mission for Referundum in Western Sahara-MINURSO)
kutekeleza majukumu yake tangu ulipoundwa mwaka 1991
3. Tunamtaka Mfalme wa Moroko kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa na
wanaharakati wanaoshikiliwa kwenye magereza mbalimbali kwenye maeneo ya
Sahara Magharibi yanayoyakalia kimabavu na Moroko.
4. Tunamtaka Mfalme wa Moroko kuacha mara moja kunyonya rasilimali za
Wasahrawi hasa madini ya phosphate na rasilimali bahari kwenye maeneo
inayoyakalia kimabavu
5. Tunamtaka Mfalme wa Moroko kuacha mara moja vitendo vya uvunjaji wa
haki za binadamu kwenye maeneo inayoyakalia kimabavu kama vile
kuwakamata wanaharakati wa Kisahrawi, kuwaweka kizuizini, kuwazuia
waangalizi wa kimataifa, waandishi wa habari na wajumbe wa jumuiya
mbalimbali za kimataifa kuingia katika maeneo ya Wasahrawi inayoyakalia
kimabavu
6. Tunamtaka Mfalme wa Moroko kuacha mara moja vitendo vya kibeberu vya
kuikalia Sahara Magharibi. Ni aibu kwa nchi moja ya Kiafrika kuitawala
nchi nyingine. Ni wakati muafaka sasa kwa Sahara Magharibi kupewa uhuru
wake
UJUMBE KWA UMOJA WA AFRIKA
1. Tunaziunga mkono jitihada mbalimbali za Umoja wa Afrika za kuitambua
na kuipigania Sahara Magharibi. Tunaitaka AU kuharakisha jitihada zake
za kuhakikisha Sahara Magharibi inakuwa huru
2. Tunautaka Umoja wa Afrika kutothubutu kuikubalia Moroko kurejea
kwenye Umoja wa Afrika mpaka pale itapoacha vitendo vyake vya kibeberu
vya kuikalia Sahara Magharibi
UJUMBE KWA UMOJA WA MATAIFA
1. Tunautaka Umoja wa Mataifa kutanua mamlaka ya MINURSO ili iweze
kutazama masuala ya haki za binadamu kwenye maeneo ya Sahara Magharibi
yanayokaliwa kimabavu na Moroko
2. Tunautaka Umoja wa Mataifa kuharakisha mchakato wa kura ya maoni ya
kuipatia Sahara Magharibi uhuru wake. Miaka 40 ya ukoloni wa Moroko
nchini Sahara Magharibi inatosha sasa!
UJUMBE KWA SERIKALI YA TANZANIA
1. Tunaunga mkono msimamo wa Tanzania wa kuendelea kuitambua na kuiunga
mkono Sahara Magharibi kwenye vyombo vya kimataifa kama vile Umoja wa
Afrika na Umoja wa Mataifa
2. Tunaitaka Serikali ya Tanzania isiyumbe katika msimamo wake kuhusu
suala la Sahara Magharibi na kamwe diplomasia ya uchumi isiwe kisingizio
cha kuizika misingi yetu ya uhuru, utu, udugu na kuwapigania wanyonge.
UJUMBE KWA WASAHRAWI
1. Sisi Ndugu zenu kutoka Tanzania, tukisukumwa na imani yetu katika
misingi ya utu, udugu na Umajumui wa Afrika, tupo nanyi bega kwa bega
katika mapambano yenu ya kuhakikisha mnapata uhuru wenu kutoka kwa
Moroko na washirika wake kutoka ng’ambo wanaowaunga mkono
2. Sisi ndugu zenu kutoka Tanzania tutaendelea kuwaunga mkono kama
alivyofanya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na viongozi
waliofuatia na wala hatutakubali kuuza utu na fahari yetu ya uhuru kwa
sababu ya ushawishi wowote ule.
Imetolewa Leo tarehe 22 Oktoba 2016
NOEL C. SHAO, Mratibu wa Mawasiliano kwa Umma, TASSC
ALPHONCE LUSAKO, Mratibu wa Haki za Binadamu, TASSC
|
No comments:
Post a Comment