Tarehe 14/10/2016 ambayo kitaifa ni siku ya kumbukumbu ya Mwl JK Nyerere iliazimishwa kitofauti na mbunge wa Viti maalum bi Anatropia Theonest.
Alifanya ziara ya Bonde la mto Msimbazi pamoja na Madiwani wa kata hizo akiwemo mh.Edwin Mwakatobe(Segerea)Edwin Mwaipaja(Liwiti) Mh.Kumbilamoto(Naibu Meya na Diwani wa Vingunguti)Pamoja na Mh.Kennedy Thomas(Kipawa)
Viongozi hawa walitembea umbali wa takribani Km 5 katika bonde hilo kuona na kushauriana na wananchi namna ya kutunza bonde hilo na kupunguza adha ya mafuriko kwa kuacha mto huo wazi ili maji yapite kwa urahisi.
Viongozi hao wamehutubia mikutano takribani 7 ya wananchi mbalimbali katika bonde hilo waliokuwa wakimiminika kuwasikiliza katika maeneo yao.
Wawakilishi hao wameshuhudia ulimaji mkubwa wa mbogamboga kiasi cha kujaza mchanga maeneo ambayo mto ungepita na kuuelekea jirani na makazi ya watu.
Uchimbaji wa mchanga unaoendelea pia umepoteza mwelekeo wa mto na kuuelekea jirani na makazi ya watu yaliyo kandokando na mto huo.
Utupaji mkubwa wa takataka katika mto huo nao umeonekana unahatarisha makazi ya wananchi hao,kwani taka hizo zimepoteza mwelekeo wa Mto huo.
Mbunge amepokea kilio kikubwa toka kwa akina mama wajane ambao nyumba zao zimeendelea kubomoka kwa ku momonyoka kwa udongo kufatuatia kazi hizo za ki uchumi.
Baada za ziara hiyo,pamoja na waheshimiwa madiwani na kamati ya mazingira iliyokochini ya mbunge huyo,ilifanya tathmini juu ya wadau(mamlaka za kata,na mtaa)pamoja na Idara zinazohusika(Halmashauri)
Madiwani wameahidi ushirikiano kupitia kamati za mazingira kukutana kwa ajiri ya kuhamasisha zoezi la usafi na upandaji wa matete na mianzi ikiwa ni plan ya muda mrefu ili kuusaidia mto huo kuwa na njia yake ya kudumu.
Katika hatua nyingine wawakilishi hawa wataanza kuomba michango ya mawe,cement na wire ngumu, kwa watu wenye mapenzi mema ili kudhibiti maeneo yanayoendelea kutishia makazi(maisha) ya watu.
Viongozi hawa wanatambua zoezi hili lilivyokuwa gumu ila wanaamini kama wananchi wakiamua kila kitu kitawezekana.
Ni ukweli usiopingika kuwa maeneo yetu ni hatarishi na kwa pamoja tungependa kuondoka kama Serikali itatupatia eneo mbadala,lakini kwa kuwa khali bado ni hii,hatuna budi kupambana na changamoto hizi ili kwa pamoja tendelee kujistil.""
Alimalizia mbunge Anatropia
Imeandaliwa na kitengo cha habari
Ofice ya Mbunge
No comments:
Post a Comment