Kamishna Sirro alizungumza na wakazi wa Mbweni
maswala ya Ulinzi na usalama kuwa ni jukumu la kila mwananchi katika mtaa wao
na kusisitiza raia wema waendelea kushirikiana na Polisi kwa kutoa taarifa za
uhakika kuhusu uhalifu unaotokea, unaoendelea kutokea na unaotarajia kutokea.
Wakati huo huo alipata fursa ya kuongelea suala la
magendo katika bandari bubu ya Mbweni ambayo imekaa katika fikra za wananchi wa
maeneo hayo na kuwataka watafute kazi nyingine za halali ili kujipatia kipato
badala ya kufanya kazi ambazo ni kinyume cha sheria za nchi yetu.
Aliwaambia
kukwepa kodi ni kosa la jinai na Jeshi la Polisi litashirikiana na TRA kuwakamata
wale ambao hawatatii sheria.
Pia aliomba wananchi kushirikiana na jeshi la Polisi
katika kuwafichua wahalifu katika maeneo ya mbweni na kushirikiana katika suala
la ulinzi katika mitaa yao kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya
kata ya Mbweni ili kuzuia vitendo vya uhalifu na uhalifu unaoweza kutokea.
Aidha kamishna Sirro aliwaomba wananchi
kushirikiana ili kumalizia kituo cha Polisi cha kata ya Mbweni ili kuondokana
na kufuata huduma mbali katika kituo kikuu cha polisi wazo Hill.
Pia alizungumzia kuhusu vikundi vinavyotokea katika
makanisa na misikiti kuwafundisha vijana mambo ya kihalifu ikiwa ni pamoja na
kuwafundisha mafunzo kama ya JUDO, KARETI NA TAIKHONDO na kuwaachisha shule. Wenye
tabia kama hizo waache mara moja, polisi wanafuatilia suala hilo ili kuwabaini
na kuwachukulia hatua watakaobainika .
Kamishna wa kanda maalum Dsm pia alipokea kero
mbalimbali kuhusiana na askari ambao sio waaminifu wamekuwa wakiwabambikizia
wananchi kesi na kudai rushwa amesema atafuatilia suala hilo na watakaobainika
atawachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.
Mwisho mkutano uliahirishwa na kamishna alitoa
namba za simu za dharura(111 na 112) ili wananchi waweze kutoa malalamiko yao
kupitia namba hizo na kutoa taarifa za kihalifu na uhalifu katika maeneo yao.
S.N.SIRRO - CP
KAMISHNA WA POLISI KANDA
MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment