Katibu wa Kamati ya Muafaka ya Yanga Mzee Ibrahim Akilimali akionyesha baadhi ya vipengele vilivyokosewa katika kukodisha timu ya Yanga kwa na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipotoa msimamo wa kamati hiyo na baadhi ya wanachama wa Yanga kuhusu ukodishwaji wa Nembo ya timu hiyo.
…………………………………………………………….
Kabla ya kufanyika mkutano Mkuu wa dharura wa klabu ya Yanga,siku ya Leo kamati ya Mwafaka wa wazee wa timu hiyo imezungumza na waandishi wa habari kuhusu maamuzi ya mwenyekiti Yusuf Manji kutaka kuitumia nembo ya Yanga kwa miaka 10 ili awe mmiliki halali.
Akizungumza katibu wa kamati hiyo Ibrahim Akilimali ,amesema kuwa kitu ambacho anataka kukifanya Manji kinapelekea kwenye vurugu kubwa kuzidi hata ile ambayo ilishawahi kutokea kipindi cha nyuma kwani atawagawa wanachama pamoja na mashabiki wanaotaka mfumo huo na wale wanaokataa mfumo huo pia.
“Sisi hatutaki kabisa kurudi kule ambapo tulipokuwepo katika migogoro ya miaka nane na mwaka 2002 ndipo tulipata mwafaka wa suluhisho na kukubaliana kuwa tutumie jina ambalo lilidhiwa na waasisi wetu na kuwa na Yanga sport club na Yanga Cooperation”alisema Akilimali
Aidha amesema kuwa Yanga kampuni ilikufa na tukaweka utaratibu wa kuwa na hisa ambazo ni 51 asilimia ni ya Yanga pamoja na asilimia 49 ni ya wanachama na tulizunguka mikoa mingi mno kwa ajili ya kuondoa migogoro,kesi na kuomba radhi wanachama wa klabu hiyo.
Hata hivyo amesema kuwa tulukuwa na mwanasheria ambaye alikuwa mwenyekiti mpaka anamaliza muda wake aliiachia Yanga Mil 200 na hapo hapo tukampata tena mwanasheria mzuri bahati mbaya Nchunga alijiuzulu baada ya kukaa miaka miwili na hatimaye tukampta bwana Manji naye akaongoza miaka miwili kwa sababu ya mahaba yetu ikabidi tuikanyange katiba kwa kumuongezea muda tena na tulimchagua tena.
“Sasa tunashangaa haijapita hata miezi nane linakuja deni la billioni 11 na laki 6 kitu ambacho kimetushutusha mno wanayanga na pia limekuja swala la kuleta hoja kuwa akodishwe Yanga na nembo ya klabu kwa muda wa mika 10 ila sisi tunasema kuwa Yanga ni kubwa sana na haiwezi kukodishwa kama masufuri ya kwenda msibani na mimi na wazee wa kamati kwa pamoja tunasema hatukubaliani na jambo hilo kwa asilimia mia”alisema Akilimali
Kwa upande wa aliyekuwa mwenyekiti wa matawi ya jiji la Dar es salaam ya Yanga,Mohammed Msumi amesema kuwa kutokana na Manji kuwa na mahitaji makubwa na timu hiyo ni vyema akakaa pembeni au kuanzisha timu yake mwenyewe na kuiacha Yanga ili iweze kujiendesha kwa mfumo wa kisasa.
“Tujiulize maswali ivi ni kwanini anataka mchakato huu ufanyike haraka huku alishawahi kusema kuwa Yanga inajiendesha kwa hasara ni mtu gani huyu anakaa sehemu ya aina hiyo na kama hawezi kufuata utaratibu wa klabu na kushindwa kufuata katiba kama anauwezo aanzishe timu yake na kuacha kutumia pesa zake kwa mabavu iili aichukue Yanga”alisema Msumari
No comments:
Post a Comment