Baada ya mapumziko ya siku moja, kikosi cha Mbeya City Fc leo kimeanza rasmi mazoezi kujiweka sawa tayari kwa mchezo mwingine wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Simba Sc uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine jumatano ijayo hii ikiwani siku tano tu baada ya suluhu ya bila kufungana na Stand United.
Muda mfupi uliopita Ofisa habari, Dismas Ten ameimbia mbeyacityfc.com kuwa, nyota kadhaa waliokosa michezo miwili iliyopita kutokana na majeraha wamekuwa sehemu ya kikosi kilichofanya mazoezi asubuhi ya leo tayari kwa kuivaa Simba Sc siku ya jumatano.
“Haruna Shamte na Sankhani Mkandawile wamekuwa sehemu ya kikosi kilichofanya mazoezi leo asubuhi, hii ni tafsiri kuwa kikosi chetu kimetimia,Simba ni timu ambayo tunaijua, hatuna shaka nao mara kadhaa wamekuja hapa wakapata kipigo, tunafahamu wamekuwa na mwanzo mzuri wa msimu lakini kucheza na City ni jambo tofauti inawalazimu kujipanga sana, waje nasisi tupo tayari” alisema.
Akiendelea zaidi Ten alisema kuwa, kikosi chake kilicheza vizuri mchezo uliopita dhidi ya Stand United na kufanikiwa kutawala mchezo wa dakika zote lakini safu ya ushambuliaji haikuwa na baati licha ya kujaribu mara kadhaa kupiga mashuti yaligonga mwamba.
“Tulikuwa na mchezo mzuri dhidi ya Stand, kwenye soka wakati mwingine bahati huwa ina nafasi yake, Simba wajiandae vya kutoasha kwa sababu tumedhamiria kufunga magoli mengi,tunajua tabia zao wanapofungwa lakini uwanja wa Sokoine una sura nyingine, jambo muhimu kwa waamuzi tunaomba wachezeshe mchezo kwa kufuata sheria 17, ili mashabiki wapate burudani na kufurahia ushindi kwa timu yao”, alimaliza.
|
No comments:
Post a Comment