Wazazi na walezi wanaosomesha watoto wao katika shule ya sekondari ya wavulana ya Abbey iliyopo Ndanda wamepigwa marufuku kuwapeleka watoto wao katika masomo ya ziada (tuition ) wakati wa likizo kwani wanachanganywa na badala yake yapewe kazi za nyumbani wafanye.
Pia, imeelezwa matokeo manzuri ya mwananfunzi yanatokana na nidhamu, mshikamano mzuri katika mazingira ya shule na nje ya shule hivyo ni jukumu la wazazi kulea watoto wao.
Agizo hilo lilitolewa jana na msaidizi wa Abate Abasia ya Ndanda na paroko wa parokia ya Ndanda,Faza Silvanus Kessy wakati wa mahafali ya saba ya kidato cha nne.
"Matokeo mazuri yanatokana na mshikamano mzuri na nidhamu ya mtoto,ni jukumu la wazazi pia katika kulea watoto , niwaonye sana na kitu kinachoitwa tuition (masomo ya ziada) kama una mtoto wako anayesoma hapa ni marufuku kumpeleka tuition na masomo ya ziada ya mitaani yanawavuruga watoto wakirudi likizo wapeni kazi za kupika, kufu, kuosha vyombo na bustani,"alisema faza Kessy
Akizungumza mkuu wa shule,Faza Augustine Ombay aliitaka serikali kutoleta siasa katika suala la elimu kwani wataangamiza taifa na kuwataka kuangalia suala la uboreshwaji miundombinu na maslahi ya wanafunzi.
"Niombe sana serikali msilete siasa katika masuala ya elimu mtaangamiza kizazi cha sasa na kijacho,sasa mkifanya mambo juu juu mtaharibu mfumo na mbele ya Mungu mtahukumiwa,nimpongeze rais kwenye suala la madawati amefaulu lakini kipaumbele kisiwe kwenye kitu kimoja tu"alisema Ombay
Aidha alisema shule hiyo inahitaji uboreshaji wa mazingira na majengo kutokana na kujengwa zamani pamoja na uchakavu wa miundombinu.
Akizungumza mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa jimbo la Ndanda, Cecil Mwambe aliwataka wazazi kuwaandalia watoto wao mazingira mazuri ya elimu ya chini ili waweze kupata nafasi ya kusoma katika shule hiyo na kuondokana na malalamiko.
"Maandalizi yanayofanyika hapa Abbey ni mazuri, elimu bora ni mchakato sisi tulio wengi hatujajiandaa ndio sababu zinazopelekea wahitimu wa ukanda huu kuwa wachache,vigezo vya kuingia Abbey sio dini wala ukabila bali ni ufaulu na nidhamu kwahiyo ndugu zangu tubadilike, "alisema Mwambe na kuongeza:
"Tusiwe watu wa kulalamika,tusidanganyane kuna elimu bora ni lazima iwe ya gharama,wazazi waunge mkono kupata elimu bora,"alisema Mwambe
Hata hivyo alimwagiza diwani wa kata ya Mwena, Nestory Chilumba kushirikiana kwa kushirikiana ma kamati ya uongozi ya shule kuona ni kwa namna gani watamaliza tatizo la upigaji wa mziki jirani na shule hiyo hali inayopelekea baadhi ya wanafunzi kutoroka.
Aidha uongozi wa shule hiyo ulimpatia mbunge huyo zawadi ya madawati 50 ambayo.
No comments:
Post a Comment