Wakati dunia ikiwa
katika kipindi cha kuhakikisha kuwa usawa katika jamii kati ya wanawake na
wanaume unafikia asilimia 50 kwa 50 nchini Tanzania imeelezwa kuwa ni asilimia
20 tu ya ardhi yote iliyosajiliwa inamilikiwa na wanawake huku wengi wao
wakiwa ni wale wanaoishi mjini jambo
ambalo linawainua wanaharakati nchini Tanzania na kuamua kukutana kujadili kwa
pamoja changamoto mbalimbali zinazowakumba wanawake katika swala zima la ardhi.
Katika kuzingatia
changamoto hiyo kubwa kwa wanawake ya upatikanaji,utumiaji na umiliki wa ardhi
na rasilimali kwa kuzingatia kufanana kwa kiasi kikubwa kwa changamoto hizo
katika ukanda wote wa Afrika,mashirika mbalimbali nchini wameandaa kongamano la
ardhi kwa wanawake wa Afrika linalojulikana kama wazo la Kilimanjaro
(Kilimanjaro initiative) kongamano ambalo limelenga kuleta sauti za wanawake wa
Africa kwa pamoja ili kuwakilisha maadhimio ya wanawake wa Africa kuhusu nini
wanataka katika kutetea mabadiliko yenye kuchochea maendeleo ya wanawake wa
Africa ikiwemo Tanzania.
Meneja kilimo na haki ya ardhi kutoka shirika la Action Aaid ambao ni washirika katika kongamano hilo Bwana Elias Mtinda akisisitiza Jambo wakati wa mkutano huo. |
Akizungumza na
wanahabari mapema leo Mkurugenzi wa TGNP kwa niaba ya mashirika shiriki wa
mkutano huo Bi Lilian Liundi amesema kuwa kongamano la ardhi la wanawake wa
Africa Mlima Kilimanjaro litaanza tarehe 13-16 October 2016 ambapo linatarajiwa
kuwa na washiriki Takribani 400 ambao ni wawakilishi wa wanawake walioko
pembezoni toka katika kanda tano za Africa ambazo ni kanda ya nchi za Africa
kusini,Africa ya mashariki,Africa ya kati,Africa ya kaskazini,na Africa
mangharibi ambapo 30 miongoni mwao Tayari wamekwishaanza kupanda mlima
Kilimanjaro kwa kusidio la kusimika madai yao juu ya ardhi kwenye kilele cha
mlima.
Ameongeza kuwa katika
mkutano huo maazimio ya wanawake wa Afrika yatawakilishwa na wawakilishi wa
wanawake kutoka kanda hizo tano za Africa na kukabidhiwa kwa wawakilishi
viongozi wa nchi pamoja na mgeni Rasmi mualikwa toka umoja wa nchi za afrika
pamoja na umoja wa mataifa.
Kongamano hilo
litakalofanyika mkoani Kilimanjaro limeandaliwa na mashirika ya ActionAid
Tanzania (AATZ),TGNP Mtandao kwa kushirikiana na International Land
Coalition,Oxfam,Wildaf,na Institute for Poverty,Land and Agrarian studies
(PLAAS).
Ros Sarwatt kutoka chama cha wanawake wajane Tanzania TAWIA akizngumza na wanahabari jinsi gani wanawake wajane wanapata matatizo ya ardhi nchini Tanzania. |
Aidha katika hatua
nyingine katika ngazi ya kitaifa wanawake Takribani mia moja wanakutana Jijiji
Dar es salaam Jumatano ya tarehe 12 mwezi huu kesho kukabidhi madai yao kwa
serikali ya Tanzania kupita Naibu waziri wa ardhi Mheshimiwa Mama Angelima
Mabula ambaye ndiye atakuwa mgeni Rasmi katika tukio Hilo litakalofanyika
katika viwanja vya TGNP.
Akizungumzia Tukio hilo Liundi amesema kuwa madai hayo ya
ngazi ya kitaifa yatajenga madai ya wanawake kikanda na hivyo kupeleka sauti ya wanawake kwa Tanzania katika jukwaa
kubwa la Africa.
PICHA ZAIDI CHINI---
PICHA ZAIDI CHINI---
No comments:
Post a Comment