Saturday, October 8, 2016

WAZEE WASTAAFU WANAWEZA KUWA MABILIONEA NA KUIBADILISHA NCHI


 Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lushoto ambaye ni Afisa Tarafa ya Lushoto,Asha Kikoti akifungua mkutano wa uzinduzi wa chama cha wazee wastaafu wilayani Lushoto kushoto ni MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Wazee wilayani humo Paul Kirua. 
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu akizungumza na wazee wastaafu wilayani Lushoto
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu akizungumza na wazee wastaafu wilayani Lushoto 
Meneja Matekelezo wa PSPF Franscis Mselemu akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa chama hicho kulia kwake ni MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu wa kwanza kuhoto katikati ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Asha Kikoti kulia ni Katibu wa chama cha wazee wastaafu wilayani Lushoto(Chawasewili)Paul Kirua
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu akimkabidhi Katibu Mkuu wa Chama cha wazee Wastaafu wilayani Lushoto (Chawasewili) Paul Kirua katiba ya Chama hicho mara baada ya kukizundua kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Asha Kikoti

Katibu Mkuu wa Chama cha wazee Wastaafu wilayani Lushoto (Chawasewili) Paul Kirua akionyesha juu katiba ya Chama hicho mara baada ya kukizunduawilayani humo kushoto ni MKURUGENZI  Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu





Wazee Wastaafu wilayani Lushoto wakimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu


Mmoja kati ya Wazee Wastaafu wilayani Lushoto,Yohana Wiliamu akiuliza swali katika mkutano huo wa uzinduzi wa chama hicho

Mzee  Mstaafu wilayani Lushoto,Judica Mandia akiuliza swali kwenye mkutano huo

Juma Rashidi ambaye ni miuongoni mwa wazee wastaafu wilayani Lushoto akiuliza swali kwa mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,Adam Mayingu



MKURUGENZI wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu amesema kuwa wazee wastaafu wanauwezo wa kuwa mabilionea na kuibadilisha nchi kwa kutengeneza ajira ,kubuni miradi inayoweza kuwaingizia kipato baada ya kulitumikia taifa katika nafasi mbalimbali walizokuwa nazo.

Alisema kwani asilimia kubwa wanaweza kuanzisha miradi mbalimbali ambayo inaweza kuwasaidia kujiongezea kipato hali itakayopelekea vijana kuweza kuinua maisha yao kitendo ambacho pia kitasaidia kuongeza pato la serikali.

Mayingu aliyasema hayo wakati wa wiki ya huduma kwa wateja Duniani ambapo mfuko huo unakutana na wadau wake ili kuweza kubaini changamoto ambazo ikiwemo kuangalia namna ya kukabiliana nazo.
Wiki hiyo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa chama cha wazee wastaafu wilayani Lushoto (Chawisewilu) chenye makazi yake mjini hapa waliokuwa wakifanya kazi na baadae kustaafu waliweza kuhudhuriwa kwa wingi na kutoa mapendekezo yao.

  “Ukiangalia wazee wastaafu wanapokuwa wamepata fedha zao za kiunua mgongo badala ya kwenda kuzitumia katika matumizi yasiyokuwa ya lazima badala yake waone namna ya kuzitumia kubuni miradi itakayokuwa chachu kwao kupitia hatua kubwa za kimaendeleo “Alisema.
“Sisi kama Mfuko wa Pensheni wa PSPF tunaunga mkono chama chenu lakini pia niwaambie Sido wapo tuzungumze nao ikiwemo kuweka utaratibu mzuri ili muweza kuona namna ya kuweza kunufaika na uwepo wao “Alisema.
“Lakini pia msisite kuwatumia wataalamu kwenye masuala mbalimbali ya ujasiriamali kwani hiyo ndio njia ambayo inaweza kuwa chachu ya kuweza kufikia malengo yenu hasa katika kipindi hiki kwa kushirikiana “Alisema.
Aidha pia aliwataka kupitia umoja wao kutumia fursa nyingi zilizopo kwenye maeneo yao kwani wanao umri wa kuishi mkubwa badala yake yaondokana na dhani ya kuwa watu wanapokuwa wakistaafu wanafariki kitendo ambacho sio hakina ukweli wowote.
Lakini pia aliwataka kutumia fursa hiyo waliyoipata kuieli misha jamii huku akiwaomba kupitia chama chao kuwahimiza vijana wao kujiunga ma mfuko wa Pensheni wa PSPF ili waweze kunufaika na mafao yanayotolewa.
Awali akizungumza wakati akifungua kikao hicho,Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Asha Kikoti aliwataka wazee wastafu kuhakikisha fedha wanazozipata za kiunua mgongo kuweka mpango mzuri wa kuzitumia kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili waweze kujiingizia kipato.
  “Kiuhalisia wazee wastaafu wanapopata fedha zao wanaona kama vile ni nyingi na kuzitumia bila kwa haraka bila kufikiria hata kuzianzishia miradi ambayo inaweza kuwasaidia kupambana na ukali wa maisha “Alisema huku akiwasisitizia wabadilike.
Sambamba na hayo aliwataka pia kuwa na mpango mzuri wa matumizi ya fedha zao za kiinua mgongo ili ziweze kuwasaidia kutumiza ndoto zao katika maisha ikiwemo kuwa na maisha mazuri.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments: