Saturday, November 26, 2016

JUKWAA LA WASTAAFU WA TAALUMA YA ELIMU WATOA RAI MABADILIKO YA MITAALA


Jukwaa la wastaafu wa taaluma ya elimu limesema ni lazima kunapokuwepo kwa mabadiliko ya mitaala ya elimu mipya ni vyema ikatengenezwa kwa kufuata sheria ya elimu na sera ya elimu ili kuepuka mgogoro wa elimu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,mwenyewekiti wa Jukwaa la wastaafu wa Taaluma ya Elimu  profesa HERME MOSHA amesema  endapo kutakuwa na mkanganyiko wa mitaala ya elimu kuandaliwa bila kufuata sheria ya elimu na sera ,basi ni makosa katika maendeleo ya elimu.

Mwenyekiti huyo wa jukwaa la wastaafu  wa taaluma ya elimu profesa MOSHA ameongeza kuwa hakuna sheria inayosema elimu ni bure,ila ni vyema wakajua kuwa sasa hakuna malipo ya ada(karo) katika mashule.

Profesa MOSHA amefafanua kuwa elimu bure ni pale unapoona mwanafunzi anapopewa kila kitu anapoingia na anapotoka shule hasa uwepo wa chakula,usafiri pamoja na mambo mengine .

Hata hivyo Jukwaa la wastaafu wa taalumu ya elimu limeeleza kuwa lengo la kuanzishwa ni kuwakutanisha wastaafu wataalumu ya elimu ili waweze kubadilishana uzoefu wa hali ubora wa elimu nchini pamoja na kujitathimini wapi Walikosea .

No comments: