Wednesday, November 16, 2016

MAJAMBAZI WATANO HATARI WAKAMATWA NA VIFAA MBALIMBALI WALIVYOPORA, FLAT SCREEN TV 4 NA VITU MBALIMBALI VILIVYONYANG’ANYWA KWA KUTUMIA NGUVU



Tarehe 13.11.2016 saa 09:30 usiku huko maeneo ya Tuwangoma mtaa wa msaki Mbagala, Kikosi Maalum cha Kupambana na ujambazi wa kutumia silaha cha Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam kilifanikiwa kuwakamata  majambazi watano baada ya kupatikana na mali ya wizi ambayo iliporwa kwa nguvu nyumbani kwa  PATRICK SAMARI miaka 35, mfanyakazi wa mamalaka ya bandari kitengo cha biashara, mkazi wa Tuwangoma ambaye alivamiwa na kundi  la majambazi wapatao 15 nyumbani kwake.

Majambazi hao walikuvunja mlango kwa matofali na kufanikiwa kuingia ndani na kuiba vitu vifuatavyo;
Bastola yenye usajili A731441 ikiwa na risasi 12 ndani ya magazine yake, kiasi cha fedha Tzs 10,180,0000/= milioni kumi na laki moja na elfu themanini, Flat Screen Tv 2 ‘54’ Laptop mbili aina ya HP, simu mbili za mkononi aina ya Samsung

Baada ya Polisi  kupata taarifa kutoka kwa PATRICK SAMARI, kikosi kazi kilianza kazi ya ufuatiliaji tarehe 14.11.016 walikamatwa watuhumiwa wafuatao;
1.PENZA SELEMAN. 2 MWARAMI NASOTO. 3 SWEED SHABANI, miaka 40, mkazi wa kinondoni Manyanya 4 MUSSA  ISMAIL miaka 27, dereva, mkazi wa Sinza na  5.SALUM TAIDINI.
Watuhumiwa wote hao walikiri kuhusika na tukio hilo na mali zote za wizi walidai walihifadhi kwa SALUM TADINI, baada ya mahojiano zaidi na upekuzi vilipatikana vifaa vyote vilivyoibiwa kama ifuatavyo;
1.Gari T533 DEQ  aina ya Toyota TI inayotumika kubebea mizigo sehemu wanazoiba.
2.Televisheni 4 aina ya Samsung
3.Laptop mbili
4.Remote control mbili
5.External driver moja.
6.Subwoofer moja
7.Deck moja
8.King’amuzi kimoja
9.Simu 2
10.Remote
Aidha katika tukio hili watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili kuonyesha Bastola waliyoiiba na kuweza kubaini matukio mengine waliyowahi kushiriki au kutenda katika maeneo mbalimbali jijini  Dsm. Upelelezi wa tukio hili unaendelea utakapokamilika watuhumiwa watapelekwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
HABARI NYINGINE KUTOKA POLISI ZIPO HAPO CHINI


KUKAMATWA  KWA WANAWAKE 4  NA  WATOTO 4  WANAOFUNDISHWA UHALIFU WA KUTUMIA SILAHA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam kupitia kikosi kazi kinachopambana na uhalifu wa kutumia silaha na ujambazi,  kimefanikiwa kukamata wanawake wanne na watoto wanne waliokuwa wamefichwa kwenye kambi. Mafanikio hayo yalipatikana baada ya kikosi kazi kufanya oparesheni kali katika maeneo mbalimbali ya misitu ya  pori la VIKINDU. watoto  hao wanne waliokuwa wametoroshwa katika familia ya ABDALA MALECK

Aidha Polisi ilipokea taarifa toka kwa mzazi mmoja wa kiume aitwaye SHABANI ABDALA MALECK mkazi wa kitunda kuwa ametoroshewa watoto wanne na mtalaka wake aitwaye SALMA MOHAMED, aliyeingizwa kwenye harakati za kigaidi.
Jitihada za pamoja na kati ya mtoa taarifa na Polisi zilifanikisha kuwakamata wanawake wanne na watoto wanne katika eneo la Kilongoni VIKINDU mkoa wa Pwani wakiwa wamekusanywa kwenye nyumba ya mtu mmoja anayeitwa  SULEIMAN, wakiwa wanafundishwa mambo ya dini na harakati za kigaidi.

Watoto hao ni 1.AISHA SHABAN miaka 13, mwanafunzi darasa la saba shule ya msingi Kizange kitunda.
2.ASHA SHABANI miaka 8, mwanafunzi darasa la nne, shule ya msingi Jitihada kitunda.
3.ABDURAHAMAN SHABANI miaka 8, mwanafunzi dara la nne, shule ya msingi Jitihada kitunda
4.FATUMA SHABANI miaka 2, mtoto wa nyumbani.

Baada ya mahojiano zaidi imeijidhihirisha kuwa wengi wao wameachishwa masomo katika  shule mbalimbali hapa nchini.baadhi ya watoto wameachishwa na wazazi /walezi wao na kuingizwa katika madrasa ambazo ndizo kambi walikokamatiwa chini ya uangalizi wa wanawake waliokamatwa pamoja nao. Sambamba na mafunzo ya madrasa pia wamekuwa wakifundishwa ukakamavu(karate/kumfuu/judo) na silaha aina ya SMG na bastola, pia wanafundishwa kupiga maeneo tete ya kummaliza mtu pumzi na kufariki haraka wakati wa mapigano (pressure point)ili kumdhibiti adui, kulenga shabaha kwa kutumia risasi, kutumia kitako cha bunduki na singe. Watoto hao wamefundishwa kuwa adui yao mkubwa ni Polisi, walinzi katika taasisi za fedha na makafri katikakujipatia kipato, wamefunzwa kupora au kunyang’anya kwa kutumia silaha na kutumia viungo
vyao.
Wanawake hao na watoto wanaendelea kushikiliwa kwa ajili ya mahojiano ili kuweza kubaini mtandao mzima katika suala hili ili kutokomeza tabia hii ya kuwachisha watoto wadogo shule na kuwaingiza katika vitendo vya uhalifu.

KUKAMATWA KWA MAGARI 4 YALIYOIBWA  NA WATUHUMIWA 4
Tarehe 10.11.2016  kikosi kazi cha Polisi kanda maalum cha kuzuia wizi magari kilifanikiwa kukamata gari T616 DCH Toyota L/cruiser mali ya JOSEPH KAYAWAYA iliyoripotiwa kuibiwa  Dsm na nyaraka kughushiwa na ikauzwa jijini Arusha, kikosi kazi kimefanikiwa kumkamata mtuhumiwa DEMESTRIOUS APOLINARY padri wa kanisa  katoliki Sumbawanga. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika atapelekwa mahakamani.

Katika tukio la pili Polisi walipokea taarifa za kuibiwa magari mawili moja aina ya SCANIA T511 AWB mali ya NELSON DANIEL mkazi wa keko juu iliibiwa keko akiwa amepaki na kupatikana Tabata na gari namba T814 DEF Mitsubish Canter mali ya HOSEA KAPULA gari hii iliibiwa sehemu isiyojulikana na mlalamikaji aligundua baada ya kununua kupewa nyaraka bandia, gari hilo lilikamatwa jijini DSM maeneo ya kigamboni.
Watuhumiwa waliokamatwa katika matukio haya mawili ni kama ifuatavyo;
1.AMANI DICKSON miaka 23, mkazi wa kigamboni
2.EXAUD MARTIN miaka 40, mkazi wa nikocheni
3.RASHID HARUNA miaka 28, mkazi wa magomeni
4.MZEE NASSIBU miaka 41, mkazi wa Yombo

Tukio lingine Polisi kupitia kikosi kazi chake kilipokea taarifa za unyang’anyi wa kutumia nguvu toka kwa  HASHIM ALLY mkazi wa kibamba kuwa ameibiwa gari lake T 724 DHZ Isuzu Canter  rangi nyeusi baada ya kukodiwa kwenda kubeba jenereta maeneo ya kibwegere  na kijana anayemfahamu kwa sura, ndipo walipofika eneo la tukio wakati akigeuza gari ili apakie mzigo huo alikabwa na vijana wapatao watatu na kumfunga kamba na kumtupa kisha kuondoka na gari. Mtuhumiwa alifanikiwa kufungua kamba na kuomba polisi na Polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja na wengine walikimbia kusikojulikana na kutelekeza gari hilo maeneo ya Bunju A. Mtuhumiwa huyo ni RAJABU ALLY miaka 35 fundi magari, mkazi wa Bunju A. mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa mara upelelezi utakapokamilika atapelekwa mahakamani.

POLISI KANDA MAALUM DSM WAMEKUSANYA TSH 587,520, 000 /= KUPITIA TOZO ZA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI
Jeshi la Polisi Kanda maalum DSM kupitia Kikosi chake cha Usalama barabarani kimekamata makosa mbalimbali ya usalama barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 09.11.2016 hadi tarehe 16.11.2016 na kuingizia serikali mapato ya ndani kama ifuatavyo;

1.     Idadi ya magari yaliyokamatwa                             - 18,073
2.    Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa                              - 1,511
3.    Daladala zilizokamatwa                                        - 6,113
4.    Magari mengine (binafsi na malori)                        - 11,960
5.    Bodaboda waliofikishwa Mahakamani                         -
kwa makosa ya kutovaa helmet na
kupakia mishkaki                                                            -
6.    Jumla ya Makosa yaliyokamatwa                          -  19,584

Jumla ya Fedha za Tozo zilizopatikana    Tzs 587,520,000/=.
 
Madereva wote wanatakiwa kutii sheria za usalama barabarani na washirikiane na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa juu ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani ili kudhibiti matukio ya ajali zinazoweza kuzuilika.

POLISI NA TRA WAFANIKIWA KUTEGUA MBINU MPYA YA WAKWEPA KODI.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania imefanikiwa kubaini mbinu mpya inayotumika na wakazi wa Mbweni ili kufanikiwa katika kupitisha bidhaa zisizolipiwa ushuru.

Aidha Polisi wakiwa pamoja na mamlaka ya Mapato Tanzania huko maeneo ya Mbweni katika njia wanazotumia kupitisha bidhaa zilizokwepa kulipiwa ushuru wanatega mbao zenye misumari,  nia yao ni kuharibu magari ya doria kwa kutandika mbao hizo chini ya barabara ili magari yapate pancha na kushindwa kuwafuatilia.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ametoa onyo kali kwa wananchi wa maeneo hayo operesheni kali inaendelea ili kuwakamata wote wanaofanya vitendo hivyo na sheria itachukua mkondo wake.



S.N.SIRRO - CP
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM




No comments: