Shangwe zikiendelea |
Wakazi wa Mbeya wameisifia sana tamasha la Mtikisiko lililoandaliwa Na kampuni ya simu za Mkononi Tigo Tanzania, wakishirikiana Na Ebony Fm lililofanyika katika uwanja wa CCM Ruanda Nzowe(Shule ya Msingi Mwenge).
Baada ya Tigo kudhamini tamasha la Fiesta katika mikoa 15, nakuibua vipaji vya chipukizi mikoani humo, Tigo waliendelea Na ahadi yao ya kupatia wanamuziki chipukizi jukwa la kuonyesha vipaji kwa kupitia tamasha la Tigo Mtikisiko, linaloratibiwa Na ebony fm katika nyanda za juu kusini.
Akiongea Na mwandishi wetu, msanii anaeibukia kwa kasi jijini Mbeya,,Zax 4Real alikuwa Na haya ya kusema "Ningependa kutoa shukrani kwa wadhimini wa Tamasha hili Tigo, kwa kuweza kunipa fursa hii ili niweze kuonyesha kipaji, Na naamini kila kampuni hapa nchini wakiiga mfano wa Tigo, basi tasnia ya mziki Tanzania itafika mbali."
Nae mkurugenzi wa Tigo Nyanda za juu Kusini, Jackson Kiswaga alisema "Sisi kama wadhamani wa Tamasha la Mtikisiko, tuko mstari wa mbele kuhakikisha wakaazi wa Mbeya wanaendelea kufaidika na huduma zetu mbali mbali ikiwemo 4G, ambayo tumeizindua rasmi katika mkoa huu,Na pia wasanii waendelea kuwa karibu Na sisi kwani kupitia jukwaa letu la Tigo Music, tunaahidi kuwawezesha wasanii wazidi kufaidika".
Tamasha la Mtikisiko chini ya Tigo lilikuwa halina kiingilio Na umati wa wakaazi walifurika kuona show kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo Roma, Stamina, Mr.Blue Na Billnass.
Msanii anaevuma Na nyimbo yake Mboga Saba, Mr.Blue , alikuwa Na haya ya kusema, "Kwa kweli watanzania wanazidi kuskliza nyimbo za ndani ya nchi kwa sababu, wasanii wamebadilishi jinsi wanavojituma katika majukwa Na pia mashabiki mnatupa nguvu ya kuzidi kufanya vizuri ".
Kawaida ya sehemu yenye mkusanyiko wa watu hapakosi wafanyabiashara wanaitumia fursa hii kutoa huduma mbalimbali, Veronica Kapinga, mkaazi wa Soweti jijini Mbeya" nimefurahi, kupata fursa, wingi wa watu umenisaidia kuuza juisi na vyakula, tunawashkuru Tigo kwa nafasi hii, hamna gharama, nimefika Na kuanza kuuza ".
Tamasha maarufu la Mtikisiko ambalo awali lilijulikana “Together Time” lilibadilishwa jina mwaka 2008 lilianza mwaka 2007 na limeendelea kukua katika kipindi chote cha miaka hiyo na kupata umaarufu kama tamasha la burudani la mwisho wa mwaka katika mikoa ya kusini.
No comments:
Post a Comment