Wednesday, November 16, 2016

QATAR AIRWAYS YAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI KWA KUCHANGIA MADAWATI KISARAWE

Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kumaliza tatizo la madawati mashuleni, Shirika la ndege linalotoa huduma ya usafirishaji wa anga la Qatar Airways nchini Tanzania limechangia msaada wa madawati 100 kwa Shule ya Msingi ya Chanzige B, iliyopo Kisarawe mkoani Pwani.

Msaada huo wa Qatar Airways ni sehemu ya mradi wa kusadia juhudi za Serikali kupitia mpango wa kuondoa uhaba wa Madawati nchini hasa shule za msingi ambapo pia kwa shirika hilo imefanya hivyo kama moja ya kurudisha shukrani kwa jamii.

Akipokea madawati hayo 100, Mbunge wa Kisarawe na Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh.Suleiman Jafo ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, ameshukuru kwa msaada huo kwani umewezesha kupunguza kero kwa wanafunzi waliokuwa wakikaa chini huku akiomba uongozi wa shule hiyo kuangalia uwezekano wa kugawa madawati hayo shule jirani pale wanapoona panafaa kutokana na uhitaji uliopo.

Aidha, Mh. Jafo ameliomba Shirika hilo la Qatar Airways kuangalia uwezekano wa kupiga tafu shule ikiwemo huduma zingine ikiwemo ujenzi wa Maktaba kama watakuwa tayari kwani tayari shule ina eneo la uwanja mkubwa wa ujenzi huo.

“Sisi watanzania. Tunafarijika na utendaji wenu Qatar Airways wa kazi hapa nchini Tanzania. Ndio maana sasa hivi tunaboresha miundombinu ya uwanja wetu wa ndege hapa nchini. Tunaamini kupitia ndege zenu tutapata watalii mbalimbali ambao watakuwa chachu ya uchumi wa Tanzania” alieleza Mh. Jafo.

Kwa upande wake Meneja wa Qatar airways Tanzania, Bw. Basek Haydar ameeleza kuwa, wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuchangia huduma za kijamii pamoja na kuimalisha usafiri wa anga kwa kuwa na safari zake mbalimbali kutokea hapa nchini Tanzania.

Tukio hilo limefanyika Novemba 14.2016 katika viwanja vya shule hiyo ya Chanzige B, ambapo pia viongozi mbalimbali walihudhuria wakkiwemo wafanyakazi wa Qatar na wawakiishi kutoka ofisi ya Doha pamoja na Dk. Amon Mkoga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Amon Mkoga Foundation, bodi ya wakurugenzi, walimu wa shule hiyo, wazazi na wanafunzi.
MO tv:
ai2a0462Mbunge wa Kisarawe na Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh.Suleiman Jafo akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa tukio hilo la kukabidhiwa madawati.

ai2a0842Baadhi ya madawati hayo
dsc_0733Mwalimu Mkuu wa shule hiyo akisoma hotuba kwa mgeni rasmi.
dsc_0752Meneja wa Qatar airways Tanzania, Bw. Basek Haydar akisoma taarifa ya Shirika hilo namna linavyosaidia jamii pamoja na shughuli zake za usafiri hapa nchini
dsc_0765Mbunge wa Kisarawe na Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh.Suleiman Jafo akitoa neno la shukrani wakati wa tukio hilo.
dsc_0771Mbunge wa Kisarawe na Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh.Suleiman Jafo, Meneja wa Qatar airways Tanzania, Bw. Basek Haydar na k. Amon Mkoga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Amon Mkoga Foundation wakiwa wameshika cheti maalum katika tukio hilo la ukabidhiwaji wa madawati.
dsc_0783Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Suleima n Jaffo akikata utepe wakati akipokea msaada wa madawati hayo 100. Anaye fuatia ni Meneja wa Qatar Tanzania Basel Haydar
ai2a0750Meneja wa Qatar Tanzania, Basel Haydar akiwa amekaa katika moja ya dawati katika hafla hiyo.
ai2a0596Picha ya pamoja baada ya kukabidhi madawati hayo
ai2a0766
QATAR TANZANIANaibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mh. Suleiman Jaffo na Meneja wa Qatar Tanzania Basel Haydar, wakipokea zawadi kutoka kwa Wanafunzi wa shule ya Msingi Chanzige B, mara baada ya Naibu Waziri Jafo kupokea msaada wa madawati 100 yaliyotolewa na Shirika la Ndege la Qatar Airways.
ai2a0681Mwalimu Mkuu akipokea zawadi kutoka shirika la Qatar
ai2a0902 ai2a0892Baadhi ya wafanyakazi wa Qatar wakifurahia kwa pamoja na baaddhi ya watoto wa shule ya hiyo ya Chanzige B, mara baada ya tukio la kukabidhiwa madawati.
ai2a0526Meneja wa Qatar Tanzania, Basel Haydar akiwa amekaa katika moja ya dawati ndani ya darasa pamoja na wanafunzi
ai2a0576Moja ya madarasa yakiwa na madawati hayo huku watoto wakiwa wamekalia
QATAR TANZANIANaibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mh. Suleiman Jaffo na Meneja wa Qatar Tanzania Basel Haydar, wakipokea zawadi kutoka kwa Wanafunzi wa shule ya Msingi Chanzige B, mara baada ya Naibu Waziri Jafo kupokea msaada wa madawati 100 yaliyotolewa na Shirika la Ndege la Qatar Airways.

No comments: