TAARIFA KWA UMMA KUTOKA MBEYA CITY FC


mccfcline-up11Baada ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili tarehe 15/11/2016 kumekuwa na taarifa nyingi, kutoka kwenye mitandao ya kijamii juu ya kuondoka kwa baadhi ya wachezaji wetu kwenda kujiunga na timu zingine pia  kusajiliwa kwa baadhi ya wachezaji kutoka timu zingine kuja kwenye kikosi chetu.

Tunapenda kuufahamisha umma kuwa taarifa zote kuhusiana na usajili mpya au kuachwa kwa wachezaji kwenye kikosi chetu zitatolewa mwisho wa mwezi huu yaani Novemba 30, kwa sasa uongozi bado unapitia na kufanyia kazi baadhi ya mambo muhimu yaliyopewa kipaumbele  kwenye ripoti ya mwalimu (kocha wetu).

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.