Wednesday, November 23, 2016

TIGO YAIPIGA "TAFU" HOSPITALI YA WILAYA YA ILEJE


Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za mkononi, Tigo-Tanzania,  Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga, (kulia) akizungumza na wananchi wa Itumba Wilaya ya Ileje, waliofika kwa ajili ya kushudia msaada waliopatiwa kutoka Tigo-Tanzania kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya hiyo, kwa niaba ya kampuni hiyo. Tigo ilikabidhi vifaa vya afya hospitalini hapo ambavyo ni mashuka, mablanketi, Goves, Jokofu na mifagio ambavyo vinagharimu kiasi cha Sh20 Milioni.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe, Joseph  Mkude (mwenye suti nyeusi) akikabidhiwa msaada wa Jokofu la kuhifadhia dawa muhimu za binadamu kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya hiyo, kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za mkononi, Tigo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga, (kulia kwake) kwa niaba ya kampuni hiyo. Tigo ilikabidhi vifaa vya afya hospitalini hapo ambavyo ni mashuka, mablanketi, Goves, Jokofu na mifagio ambavyo vinagharimu kiasi cha Sh20 Milioni.


Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe, Joseph  Mkude (aliyechuchumaa) akichoma moto takataka baada ya kuzikusanya katika usafi walioufanya pamoja na maofisa wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo-Tanzania, katika Hospitali ya Wilaya ya Ileje, baada ya Tigo-Tanzania kukabidhi msaada wa vifaa tiba hospitalini hapo vinavyogharimu kiasi cha 20 Milioni.

Usafi ukiendelea 

Wananchi wa Itumba Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe, wakifuatilia matukio wakati Kampuni ya simu za mkononi Tigo-Tanzania wakaikabidhi vifaa tiba kwa uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Ileje, ambavyovinagharimu kiasi cha Sh20 Milioni.

No comments: