Tangu kutokea sintofahamu juu ya wapi alipo kada maarufu wa chadema Ben saanane kumekuwa na minongono mingi juu yake huku mengine yakihusishwa na kile kinachoitwa kutekwa na wapinzani wake kisiasa,huku wengine wakiamini kuwa Kada Huyo amejihifadhi mahali ili kitengeneza jina lake kisiasa.
Gazeti la mwanahalisi ambalo linaongozwa na Mbunge wa chadema Ubungo na mwandishi nguli wa uchunguzi Said Kubenea wiki hii limebadilisha upepo wa sakata hilo baada ya kudai kuwa Kada huyo hajapotea na yupo mtaani anaonekana akipata kahawa na rafiki zake.
SOMA BAADHI YA SENTENS ZA MAKALA HIYO HAPA
UTATA kuhusu kutoonekana kwa Bernard Saanane, msaidizi wa masuala ya siasa wa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe sasa unazidi kuongezeka. Wanaandika Waandishi Wetu …. (endelea).
Taarifa zinasema Saanane ambaye haonekani nyumbani wala kazini, anaonekana kwa marafiki zake mitaani. Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya Chadema amesema, “Nina wasiwasi kama siyo mkakati binafsi wa kisiasa.
Kijana Saanane amekuwa akionesha kutaka kukwea madarakani haraka hata nje ya taratibu. ”
Baada ya makala hiyo makada mbalimbali wa chadema akiwemo huyo maarufu kama Malisa ameamua kuandika hitaji lake la kutaka polisi kumkamata mara moja kada mwenzao Said Kubenea kwa ajili ya kueleza ukweli juu ya kuonekana kwa Ben Saanane.
SOMA ALICHOKIANDIKA
Taarifa za Mhe.Kubenea kwamba Ben yupo mtaani anarandaranda na kujificha kwa rafiki zake, ni
taarifa zinazopaswa kufanyiwa kazi na Jeshi la Polisi na uongozi wa Chadema. Takribani mwezi mmoja sasa polisi na Uongozi wa Chadema umetoa taarifa rasmi za kumtafuta Ben. Leo Kubenea anasema Ben yupo mtaani, anaonekana kwenye vijiwe vya kahawa.
Ni vizuri Polisi wakamkamata Kubenea aeleze ni mitaa ipi Ben alionekana, na ni vijiwe vipi vya kahawa alivyokutwa. Je alikua na nani? ni siku gani? aliyemuona ni nani? na kwanini alipomuona hakutoa taarifa polisi? Na kwa kuwa Kubenea anajua polisi wanamtafuta kwanini alipojua Ben yupo mtaani hakwenda kuripoti polisi ili awasaidie ktk kufanya uchunguzi? Kwanini Kubenea anawaacha Polisi watumie rasilimali kubwa kumtafuta Ben wakati anajua Ben amejificha ili kujipatia umaarufu wa kisiasa?
Kubenea anasema Ben anatafuta umaarufu, je ni umaarufu gani wa kujipoteza? Ili iweje? Kwa faida ya nani? Kwamba Ben akijipoteza ndo anakua maarufu? Halafu huo umaarufu unamsaidiaje? Kugombea nafasi ya uongozi kwenye chama? Ni nafasi gani ambayo mtu huchaguliwa kwa kujipoteza? Na ni akina nani watakua wajinga wa kumpa mtu kura kwa sababu tu alijipoteza? Hivi kujipoteza kwa Ben kunamuongezea kura au kunampunguzia?
Kama kweli Ben yupo mtaani, je Kubenea haoni kuweka taarifa gazetini ni kumfanya azidi kujificha? Kwanini asingewaarifu polisi kwanza wamkamate then ndo aweke gazetini? Na hao marafiki zake Ben waliomficha huko mtaani ni mahiri wa ujasusi kiasi gani? Je wamewazidi akili polisi, usalama wa taifa na intelijensia ya Chadema? Je Kubenea kuandika habari bila kujibu maswali muhimu (5Ws +H) haoni kunaifanya habari hiyo kukosa uhalali wa kuaminika mbele ya jamii?
Na kwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema Mhe.Freeman Mbowe alitamka hadharani kuwa kuna uwezekano Ben ametekwa, je Kubenea kusema Ben kajificha haoni anamfanya Mbowe kuonekana ameshiriki kumficha Ben? Kwa kuwa Kubenea ameshindwa kutaja vyanzo vyake vya habari haoni habari hiyo inaweza kuonekana ni ya kutunga maana haina credible source? Je ikija kubainika kuwa Ben ametekwa au amekufa, je Kubenea haoni kwamba atakua amewakosea sana watanzania, kuikosea familia ya Ben, na hata nafsi yake mwenyewe?
Sisemi kuwa Ben hawezi jificha, as a human being anaweza kufanya hivyo na ikibainika kajificha nashauri achukuliwe hatua kali za kisheria. Lakini ukweli ni kuwa habari ya Kubenea imeacha maswali mengi kuliko majibu.
Nahofia Kubenea asije kuwa ameandika habari hiyo kwa chuki binafsi dhidi ya Ben halafu baadae akaja kujuta. Nafahamu ugomvi binafsi kati ya Ben na Kubenea uliosababishwa na tofauti za kisiasa. Kuna mengi yalitokea ambayo siwezi kuyasema yote hapa lakini Ben na Kubenea wamewahi kunyukana kwa nyakati tofauti kwa sababu mbalimbali (ushahidi wa maandishi yao wakinyukana upo).
Sasa isije kuwa Kubenea anaendeleza mnyukano kati yake na Ben akasahau suala la uhai wa mtu ni muhimu kuliko tofauti zao za kisiasa. Ikibainika Ben amejificha Kubenea atakua shujaa kwenye hili, lakini ikija kubainika kuwa Ben amekufa, kuuawa au kutekwa, dhamiri ya Kubenea itamhukumu maisha yake yote. Ni vizuri kuwa na akiba ya maneno.!
No comments:
Post a Comment