Moja ya ndege ambayo serikali imedhamiria kununua inayotarajiwa kuwasili nchini Juni 2018 ni Boeing 787 Dremaliner. Ndege hii ni ya kisasa ambapo ndege ya kwanza ya aina hii ilianza kuruka mwaka 2009 ambapo inauwezo wa kwenye maili 567 (km 912.5) kwa saa moja.
Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James. Baada ya Mazungumzo hayo Rais Magufuli alisema Serikali yake ya Awamu ya Tano imedhamiria kununua ndege nyingine nne zikiwemo ndege kubwa 3 ambazo zitasaidia kuinua uchumi wa nchi kwa kuwezesha watalii kuja hapa nchini moja kwa moja kutoka nchi zao.
Hapa chini ni video kutoka Shirika la Ndege la Uingereza wakikuonyesha namna ndege hiyo ilivyo pamoja na ubora wake.
TAZAMA VIDEO:
No comments:
Post a Comment