Diwani wa Kata ya Mbagala Kilungule, Said Fella pamoja na Taasisi ya Upendo ni Mimi ya leo wamejitokeza katika kuchangia damu katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusaidia wahitaji wa huduma hiyo.
Taasisi ya Upendo ni Mimi ina jumla ya wanachama hai 20, ikiwa na lengo la kutoa misaada wa makundi maalumu wakiweo watoto yatima na walemavu, kutoa elimu ya kuzui na kujijkinga na matumizi ya dawa za kulevya, ndoa za utotoni na kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi.
“Sisi kama Upendo ni Mimi tumejipanga kurudisha tumaini na faraja kwa makundi maalumu kwa sababu wamesahaulika na ndiyo maana leo tumeamua kujitolea kuchangia damu katika hospitali yetu, tunamshukuru Diwani Fella kwa ushirikiano wake,” alisema Meneja Mradi wa Upendo ni mimi, Hamza Issa.
Jumla ya wachangiaji 60 ambao walijitokeza kuchangia damu akiwemo msanii Kayumba Juma, Salam TMK, Omarly Clyton na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment