MAANDALIZI kuelekea dakika 90 za mchezo namba 130 wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya Mbeya City fc na wageni Toto African ya Mwanza uliopangwa kuchezwa kesho kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa yamekamilika.
Akizungumza na mbeyacityfc.com muda mfupi uliopita meneja wa kikosi cha City, Godfrey Katepa amesema kuwa hali za nyota wa timu yake iko vizuri kabisa tayari kwa mchezo huo wa kesho, jambo linaloashiria kuwa hakuna kitakachoizua City kuibuka na ushindi dhidi ya timu hiyo kutoka Mwanza.
Hali ya kikosi chetu ni zuri kabisa, hakuna mchezaji yoyote aliye majeruhi, Haruna shamte aliyekuwa na maumivu ya kifundo cha mguu amerejea kikosi baada ya matibabu ya siku kadhaa jopo la madaktari wetu wametuthibitishia kuwa yuko sawa tayari wa mchezo wa kesho,ni wazi hakuna kinachotuzuia kushinda mchezo huo alisema.
Kuhusu suala la wachezaji wa kigeni, Katepa alisema kuwa tayari hatua zishachukuliwa hivyo mashabiki wa City wasiwe na wasiwasi juu ya kuwepo kikosini kwa wachezaji wao wanaotoka nje ya nchi.
Viongozi wameshalichukulia hatua, kila kitu kishakamilishwa hivyo niwatoe wasiwasi mashabiki juu ya kocha na wachezaji wao kutoka nje,taratibu ziko safi na watashiriki mchezo wa kesho, waje uwanjani kwa wingi kwa ajili ya kuisapoti timu yao na wategemee ushindi kwa sababu tunataka kushinda ili tutoke kwenye nafasi tulipo sasa katika msimamo wa ligi na kusogea juu zaidi.
Akiendelea zaidi Katepa aligusia suala Mrisho Ngassa kuwa bado halijakamilika kwa maana ya kufika kwa ITC yake lakini uongozi unaendelea kufanya mawasiliano na klabu ya Fanja ya Oman kuhakikisha suala hilo linakamilika ili nyota huyo aweze kuitumikia City kwenye michezo inayofuata.
Ni wazi ataukosa mchezo huu, suala lake bado halijakamilika, jambo muhimu ni kuwa uongozi bado unaendelea kufanya mawasiliano na klabu ya Fanja kuhakikisha linakamilika ili aweze kuichezea timu yake mpya kwenye michezo ijayo, awali walitutumia TPO pekee, hivyo tunasubiri RELEASE LETTER kutoka kwao ili tuweze kupata ITC kwa mujibu wa taratibu, ilikuwa watutumia jana lakini mtu ambaye alipaswa kufanya hiyo kazi alikuwa nje ya Oman na anarejea leo.Hatuna msuguano wowote na Fanja kama inavyoripotiwa mawasialino kati yetu ni mazuri kama ilivyo kwa Tff na chama cha mpira cha Oman hivyo siku si nyingi suala hili litafikia mwisho alimaliza.
No comments:
Post a Comment