Wakati nchini Tanzania wanasheria
pamoja na wadau mbalimbali wa maswala ya sheria wakeiendelea kuishawishi serikali
hiyo kuifanyia marekebisho sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 ya nchini Tanzania hatimaye
Wizara ya Katiba na sharia kwa kushirikiana na mashirika ya Action Aid na TGNP wamewakutanisha wadau
mbalimbali kutoka asasi za kiraia,wanazuoni na wanahabari na kuwapa nafasi ya
kupitia sheria hiyo na kupendekeza baadhi ya marekebisho ambayo wanadhani
yanastahili kufanyika katika sheria hiyo.
Sheria ya Ndoa nchini
Tanzania ni moja kati ya sheria ambazo zimekuwa zikizua gumzo kwa kipindi
kirefu hadi kufikia hatua ya baadhi ya wanaharakati kufungua kesi mahakamani
kupinga baadhi ya vifungu ambavyo wanadai vimekuwa vikikinzana na sharia nyingine
ziliozopo nchini.
Katika mkutano mapitio
ya sheria hiyo ambao umemalizika Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo
wanasheria kutoka maeneo mbalalimbali,wadau kutoka katika asasi za kiraia,wanahabari
na pia kuhudhuriwa na wadau wakubwa wa sheria hiyo kutoka wizara ya katiba na sheria
wametumia muda mwingi kuipitia sharia hiyo kifungu kwa kifungu na kutoa maoni
na maoendekezo yao.
Akizungumza
na mwandishi wa mtandao huu mwakilishi kutoka serikalini aliyekuwa katika kikao
hicho Bwana Cazmiry Sabath alisema kuwa lengo kuu la kuwakutanisha wadau hao ni
kuchukua maoni ya jinsi gani ya kutekebisha na kuifanya sheria ya ndoa nchini
Tanzania kuwa bora Zaidi tofauti na sasa ambapo imekuwa ikilalamikiwa na wadau
mbalimbali huku akisema ni mwendelezo wa kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii
kusikia wanasema nini juu ya sheria hiyo
Baadhi
ya vifungu ambavyo vilijadiliwa kwa kina na kuonekana vinahitaji marekebisho ni
pamoja na kifungu cha 69-71 kinachozngumzia kuhusu mtu kuwa na uwezo wa
kumshtaki mwenzake ambaye aliahidi kumuoa na baadae kuvunja ahadi hiyo ambapo
wadaun hao walitoa mapendekezo kadhaa huku wengine wakitaka kifungu hicho
kiweke wazi ni lini ahadi ya ndoa inaanza kuhesabiwa,Kifungu cha 72 ambacho
kinamtaka mtu akikamatwa Ugoni alipe faini ya shilingi laki mbili ambapo wadau
hao walidai kuwa faini hiyo ni udhalilishaji kwa kuwa wapo watu wenye uwezo wa
kulipa hivyo hiyo sio dawa ya kupunguza matukio hayo bali ni kuyaongeza Zaidi.
Sheria
ya ndoa imekuwa ikizua gumzo hasa katika kifungu kinachozungumzia umri wa mtu
kuolewa ambapo kimekuwa kikikinzana na sheria ya mtoto ambayo inamtaja mtoto kuwa
ni mtu mwenye umri wa miaka 18 kushuka chini huku sheria ya ndoa ikisema mtu
anaweza kuolewa hadi na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi jambo ambalo wanaharakati
mbalimbali wapo mahakamani kutetea sakata hilo.
Katika
mkutano huo ulioandaliwa na Wizara ya katiba na sheria kwa kushirikiana na Mtandao wa TGNP na USAID wasomi mbalimbali
walitoa maoni yao akiwemo Cazmiry Sabath kutoka Serikalini,Scholastica Haule,
kutoka Action Aid Tz,Dr Hashir Twaibu Abdallah( kutoka kitivo cha sharia UDSM)
Mhadhiri na mwanasheria. Richard Mbonde huyu ndiye mwenyekiti wa kikao na Bwana
Michael Mushi, ambaye ni wakili kutoka kampuni ya ushauri wa miradi iliyopo
shekilango .
No comments:
Post a Comment