Wednesday, January 18, 2017

Baada ya Mtwara kutajwa Kuwa Hafifu Kielimu,Hii ni Mipango Mipya Kutoka Tandahimba

Wanafunzi wa shule ya Secondary Naputa Iliyopo Tandahimba mkoa wa Mtwara ambao ni mkoa kati ya kumi Hafifu Kitaifa
 Tandahimba.Kutokana na matokeo ya kidato cha pili kuwa mabaya halmashuri ya wilaya ya Tandahimba imeamua kutenga bajeti  ya Sh 10 milioni ili kukipa nguvu kitengo cha elimu kinachokagua masuala ya elimu.


Akizungumza katika kikao cha bajeti ya mwaka 2017/2018 mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka ambaye katika mkoa wa Mtwara imetoa shule nne zilizofanya vibaya kati ya tisa,alisema kitengo hicho kimekuwa kikishindwa kufanya kazi ipasavyo hivyo wameamua kukiongezea nguvu ili kuinua elimu.

Hata hivyo halmashauri hiyo imetenga kiasi cha Sh 10milioni kwaajili ya kuongezea nguvu kamati ya nidhamu ya walimu  ili kuwajibika ipasavyo sambamba na kutengea Sh 480 milioni kuboresha miundombunu ya shule pamoja na kiasi cha Sh 78 milioni zimetengwa kuwezesha watoto kupata chakula shuleni.

"Halmashauri katika bajeti ya mwaka 2017/18 tayari tumetenga kiasi cha pesa Sh 10 milioni ili kukipa nguvu kitengo cha elimu kinachokagua elimu kwasababu tumeoana wanashindwa kuwajibika ipasavyo  kutokana na ufinhy wa bajeti, ambapo pia tumetenga bajeti kwaajili ya kamati ya nidhamu ya walimu iili waweze kufanya kazi yao vizuri kwani kutokana na wo kutofanya kazi yao vizuri kunapelekea baadhi ya walimu kutowajibika ipasavyo,"alisema Msomoka

Aidha alisema sababu nyingine zinaopelekea shule kufanya vibaya ni hamasa duni kwa wananfunzi  pamoja na kukosa chakula hali inayopelekea  washindwe  kuhudhuria masomo ipasavyo ambapo tayari wametenga bajeti  ya Sh 78 milioni.

"Ni kweli tumefanya vibaya lakini tumeweza kutenga Sh  10 milioni kukipa nguvu kitengo cha elimu kinachokagua  kwasababu kimekuwa kikikabiliwa na ufinyu wa bajeti hivyo kupelekea washindwe kufanya majukumu  yao vizuri, pamoja na ile kamati ya nidhamu ya walimu tumewaongezea kiasi cha Sh 10 milioni ili kuwapa nguvu,”alisema Msomoka

Akizungumzia hali hiyo mmoja wa walimu kutoka shule ya sekondari ya Naputa iliyofanya vibaya, Rajabu Nampoto alisema hali hiyo imechangiwa na uhaba wa walimu wa sayansi huku baadhi ya masomo yenye walimu wakilazimika kufundisha vipindi vingi zaidi ya wastani unaotakiwa.

Alisema kwenye masomo kama biology  hawakuwa na walimu huku somo kama Fizikia na Hisababti yakifundishwa na mwalimu mmoja kuanzia kidato cha kwanza hadi  nne.

"Sababu zipo nyingi kama ukosefu wa walimu wa Sayansi na hata mwalimu aliyepo analazimika kufundisha vipindi  57 kwa wiki kwani anafundisha kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne,"alisema Mwal Nampoto

Aidha alizitaja sababu nyingine ni baadhi ya wananfunzi kutojua kusoma, kuandika na kuhesabu hivyo kupelekea baadhi ya walimu kutotekeleza mitahala kwasababu wanalazimika kuwafundisha kusoma kwanza.

"Sababu zipo nyingi kama utoro mfano hawa ambao matokeo yao ndio yametangazwa jana kuna ambaye hakufanya mitihani yote kutokana utoro lakini baadhi wamekosa stadi za kusoma,kuandika na kuhesabu kwahiyo tunapowapokea lakini baadhi yao baada ya mitihani wanajiengua wenyewe na wale wanaobaki inabidi tuwasaidie,"alisema mwalimu Nampoto

Akizungumza katika kikao cha kupitisha bajeti  mwenyekiti wa halmashauri ya Tandahimba,Namkulya Selemani aliwataka madiwani kwenda kufikiria na kuona sababu za kufeli ni nini kabla ya kuitisha kikao cha dharura  kwani asilia kubwa ya shule zilizofanya vibaya miundombunu yake imekamilika.

"Haya matokeo sio mazuri, yameniuma sana inatakiwa tuitishe kikao cha dharura  kulijadili hili haiwezekani ile shule yenye walimu wachache ndio imefanya vizuri na zile shule ambazo zina walimu wengi na miundombinu yake imekamilika ndio wanaoingia katika kumi zilizofanya vibaya,madiwani naomba mnapokwenda huko mkaangalie sababu ni nini kabla hatujakutana kujadili, "alisema Namkulya

No comments: