Thursday, January 26, 2017

CHADEMA WAPATA MSIBA KANDA YA VICTORIA

Makamanda, tunasikitika kuwatangazia chama kimepoteza kamanda mwenzetu Timotheo Paul (28) ambaye alifariki jana hospitalini Bugando kutokana na majeraha aliyopata akiwa kwenye kampeni Kata ya Kimwani, Muleba Kagera. 


Alikuwa kiongozi wa Bavicha katika kata hiyo. Kutokana na mazingira ya kifo chake, chama ngazi ya kanda ya ziwa Viktoria kimesafirisha mwili wa marehemu kwa kutumia gari la kanda leo alasiri. 

Hivi ninavyoandika, msafara ndio unakaribia Kimwani. Waliosindikiza mwili huo wakiambatana na ndugu wa marehemu, ni Meshack Micus, Katibu wa Kanda, na Khalid Selemani, ofisa katika ofisi ya kanda. 

Kamanda Timotheo amefia kazini. Amekufa kwa heshima. Tumwombee huko aendako alikotangulia. Mungu amweke mahali pema! 

Taarifa nyingine zitafuata kadiri zitakavyotufikia. 

Hapo hapo, huko huko Kimwani, kijana mwingine amezikwa leo. Huyo alifariki kwa ajali siku ya uchaguzi. 

Kutoka Nkome, Geita, kuna kijana aliyejiua Jumapili siku ya uchaguzi baada ya matokeo, alipomwona mama yake mzazi anashangilia ushindi wa CCM. Kijana (jina lake halijapatikana bado ). Alijinyonga . 

Mungu awape faraja wafiwa!. Na aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. AMEEN 

............................................ 
ANSBERT NGURUMO 
Makamu Mwenyekiti CHADEMA 

Kanda ya Victoria

No comments: