Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA) imetangaza bei mpya za nishati ya mafuta zitakazoanza kutumika leo Jumatano huku bei ya mafuta ya taa na dizeli ikiwa imeshuka kwa wastani wa shilingi 66 kwa lita.
Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Felix Ngamlagosi inaonesha kuwa kwa wastani kumekuwa na ongezeko dogo sana la bei ya mafuta ya petroli ambayo kwa jiji la Dar es Salaam bado itauzwa kwa bei ile ile ilivyokuwa mwezi uliopita.
Hata hivyo, taarifa hiyo imetoa ruhusa kwa wauzaji wa jumla na rejareja wa mafuta nchini kuuza bidhaa hiyo kwa bei ndogo chini ya bei elekezi iliyotangazwa na mamlaka hiyo kama njia ya kuchochea ushindani baina ya wauzaji wa mafuta nchini.A
No comments:
Post a Comment