Saturday, January 28, 2017

INTER SCHOOL DEBATE COMPETITION 2017 YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM



Wanafunzi mbalimbali wa shule za Seciondaruy jana walipata nafasi ya kushiriki katika mashiundano makubwa ya Interschool Debate Compitition yaliyofanyika Jijini Dar es salaam katika Viwanja vya sabasaba ambapo katika mashindano hayo wanafunzi hao walikuwa na nafasi ya kuchangamsha Bongo zao kwa Kuchangia Mada mbalimbali huku washindi wakijinyakulia Zawadi mbalimbali zikiwemo Vitabu kwa ajili ya masomo yao
Akizungumza na Mtandao Huu wa HABARI24 BLOG Mwanzilishi  na Mwaandaji wa mashindano hayo Bwana Shukuru Ngongoje ameeleza kuwa mashindano haya yanalenga kuwajenga wanafunzi wa Tanzania hususani wa shule za Secondary katika kujiamini na kuwa na uwezo wa Kutoa hoja na kukubali hoja jambo ambalo litawasaidia hata baada ya maisha ya uwanafunzi kwa kuwa dunia ya sasa imekuwa ikihitaji wanafunzi ambao wanauwezo wa kujieleza na kutoa hoja zenye nguvu.

Amezitaja shule ambazo zilishindanishwa jana katika INTERSCHOOL DEBATE COMPITATION kuwa ni Tuisiime Secondary school,Jitegemee Secndary,St Maria Salome,Mwandege Boys,Gome secondary,Kibasila Secondary ambapo washindi watatu wa Juu ambao ni Best Speaker wakiondoka na Zawadi kedekede yakiwemo madaftari kwa ajili ya masomo yao mashuleni.

Mashindano hayo yamepewa Nguvu na Masumini Printways and stationary, pamoja na Channel Ten na magic Fm.
PICHA ZAIDI BONYEZA CHINI



No comments: