Saturday, January 21, 2017

Jeshi la Polisi Lavamia Mkutano wa ACT Wazalendo kwa Lengo la Kumkamata Zitto Kabwe




Taarifa tulizopokea kutoka Kahama ni kuwa Jeshi la Polisi limevamia Mkutano wa Kampeni wa ACT Wazalendo katika Kata ya Isagehe kwa lengo la kumkamata Kiongozi wa Chama, ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto. Hata hivyo, bado hawajamkamata kwa kuwa alishaondoka katika eneo la mkutano mara alipomaliza kuhutubia lakini wanashilikia moja ya magari yaliyoko kwenye msafara wake.

Tunaamini hatua hii ya Jeshi la Polisi inatokana na msimamo wa chama chetu juu ya tishio la baa la njaa nchini na mambo mengine ya kitaifa, pamoja na kuzidiwa kwa CCM katika kampeni zinazoendelea katika Kata ya Isagehe. 

Tunaendelea Kufuatilia kinachoendelea na tutaujulisha umma kila hatua. Katika hatua hii tunalaani hatua hizi za kuendelea kugandamiza Demokrasia na juhudi Ovu za Serikali ya CCM za kutaka kulazimisha Ushindi katika maeneo ambayo chama chao hakikubaliki. 

Tunawasihi wanachama wetu na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa watulivu tukiendelea kufuatilia jambo hili. 

Ado Shaibu
Katibu - Kamati ya Itikadi, Mawasiliano ya Umma na Uenezi
Januari 21, 2017

No comments: