Sunday, January 29, 2017

Picha 22: JINSI WACHIMBAJI 15 WALIOFUNIKWA UDONGO MGODINI GEITA WALIVYOOKOLEWA WAKIWA HAI


Mungu Mkubwa!! Ndivyo unaweza kusema...Hatimaye wachimbaji wa madini 15 waliokuwa wamefunikwa na udongo katika mgodi wa dhahabu wa RZ Union mkoani Geita wameokolewa wakiwa hai na wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Geita.

Picha zote na Joel Maduka-Malunde1 blog Geita
Wachimbaji hao wakipatiwa huduma baada kuokolewa

Watu hao akiwemo raia wa China mmoja walifukiwa na kifusi juzi usiku baada ya udongo kukatika na kuziba mlango waliokuwa wakitumia kuingia na kutoka na uokoaji unaendelea kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya uokoaji.
Wachimbaji hao wakiwa wamelala chini mara baada ya kuokolewa kutoka chini ya ardhi katika mgodi wa dhahabu wa RZ Union mkoani Geita kufuatia kukwama tangu juzi kwa kifusi kuziba njia ya kutokea na kushindwa kutoka nje.
Mchimbaji akitoka chini ya ardhi baada ya kuokolewa
Uokoaji ukiendelea
Raia wa China(aliyevaa nguo nyeupe) baada ya kutoka ardhini
Raia wa China baada ya kutolewa ardhini













Picha zote na Joel Maduka-Malunde1 blog Geita

No comments: