Tuesday, January 24, 2017

WANAHABARI WATEMBELEA SHAMBA LA ZABIBU KITUO CHA UTAFITI WA KILIMO MAKUTUPORA DODOMA

 Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati walipotembelea shamba la utafiti wa zabibu katika Kituo cha Utafiti  wa Kilimo Makutupora mkoani Dodoma leo.
 safari kuelekea shamba la zabibu ikiendelea.
 Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso (katikati), akitoa ufafanuzi wa kilimo cha zabibu kwa wanahabari. Kushoto Mtafiti Msaidizi wa kituo hicho, Richard Malle na kulia ni Mtafiti Andekelile Mwamahonje.
 Wanahabari wakiwa katika shamba hilo.
 Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso (kushoto), akionesha mche wa zabibu uliostawi vizuri.
 Wanahabari wakiangalia shamba hilo.
Mtafiti Msaidizi wa kituo hicho, Richard Malle akitoa ufafanuzi wa kilimo cha zao la zabibu kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
Na Dotto Mwaibale, Dodoma

VIJANA wametakiwa wajiunge kwenye vikundi na kuanzisha mashamba ya kilimo cha zabibu ili wajipatie kipato badala ya kukaa vijiweni.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mroso wakati akizungumza na wanahabari waliotembelea shamba la zabibu katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mkoani Dodoma leo.


"Mwito wangu kwa vijana waanzishe vikundi vitakavyoweza kuwasaidia kuanzisha mashamba ya zabibu ili wajiongezee kipato mikopo ya kuwezeshwa ipo" alisema Mroso.

Alisema mtaji wa kuanzisha shamba la zabibu ni kuanzia sh. milioni tatu hadi nne ambapo baada ya miaka mitatu au minne mkulima anaanza kunufaika na kilimo hicho.

Alisema katika kuinua pato la taifa na la mtu mmoja mmoja serikali imeaanzisha mashamba ya zabibu maeneo mbalimbali mkoani humo ambapo katika Halmshauri ya Wilaya ya Chamwino kuna shamba la ekari 296, katika Kijiji cha Kamaiti wilayani Bahi kuna shamba la ekari 170 na Manispaa ya Dodoma katika Kijiji cha Gawaye kuna ekari 100 ambapo kila mwananchi hasa vijana wamepatiwa ekari moja kuziendeleza.

Alitaja aina za zabibu zinazolimwa katika maeneo hayo kuwa ni za mezani, mvinyo na kukausha ambazo soko lake linapatikana wakati wote.


No comments: