Thursday, January 5, 2017

ZITTO KABWE KUUNGURUMA KAHAMA NA GEITA KUANZIA KESHO

Mbunge wa kigoma Mjini na Kiongozi wa chama cha ACT WAZALENDO Mh ZITTO KABWE anatarajiwa Kufanya Ziara ya kisiasa katika mikoa kadhaa nchini ambapo katika ziara hiyo atapata nafasi ya kufanya mikutano ya hadhara na kuzungumza na wananchi.

 Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka kwa Afisa wa Habari wa Chama Hicho Abdala Khamis kuja kwenye mtandao huu Kiongozi huyo anataraji kufanya ziara katika mikoa kadhaa ambapo Ratiba yake inasomeka kama inavyoonekana hapo chini,

06/01/2017 - Geita 
-Mkutano

07/01/2017 - Kahama 
-Kukutana na wajumbe wa vituo vya kupigia kura(Asubuhi) 
-Mkutano (Jioni)

08/01/2017 - Kahama 
-Kufungua matawi 
-Mkutano

09/01/2017 - Geita 
-Kufungua matawi 
-Mkutano.

No comments: