Na Exaud Mtei Dar es
salaam
Baada ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli jana kuagiza kusikilizwa
na kusaidiwa kwa mwanamke mjane ambaye alileta malalamiko yake ya kudhulumiwa
mali za Mumewe jana katika maadhimisho ya siku ya Haki Duniani,Hatimaye chama
cha wanawake wajane nchini Tanzania TAWIA wameibuka na kutoa ya moyoni kuhusu
swala hilo huku pia wakipongeza hatua za haraka zilizochukuliwa na Mh Rais.
Akizungumza na
wanahabari Mapema leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Chama hicho Rose
Sarwatt amesema kuwa chama hicho kimefarijika sana na hatua za Rais kuanza
kuwajali wajane wa nchi hii jambo ambalo walilipigia kelele kwa muda Mrefu
katika serikali zilizopita ambapo kwa Serikali ya Awamu ya Tano imeonyesha njia
na matumaini mapya kwa wajane.
Aidha pamoja na Pongezi
hizo Mkurugenzi huyo ametuma ombi maalum kwa Rais ambapo amesema kuwa
kushughulika na Tatizo la mtu mmoja ni sahihi lakini Mh Rais akumbuke kuwa
mjane huyo ni mmoja kati ya wajane Zaidi ya laki saba nchi nzima kwa mujibu wa
ofisi ya Takwimu ya mwaka 2012 hivyo kumtaka Rais kuanza kuwasikiliza wajane
wote nchini ili kupunguza adha kubwa wanayoipata pindi tu ambapo wanaondokewa
na wanaume zao ambapo hukumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuzulumiwa
mali zao.
Mkurugenzi wa Chama hicho Rose Sarwatt akizngumza na wanahabari mapema leo |
Aidha wanawake hao
wameiomba serikali kuanzisha mahakama ya familia itakayosimamia kesi zote za
masuala ya familia ikiwemo kesi za mirathi jambo ambali wamesema kuwa litaondoa
msongamano wa kesi za wajane zilizojaa katika mahakama mbalimbali nchini
Tanzania ambazo pia zimedumu kwa muda mrefu bila kupata ufumbuzi.
Hata hivyo wajane hao
wameomba kufanyiwa kwa marekebisho sheria ya mirathi ya mwaka 1963 ambapo
amesema kuwa kama ilivyo kwa sheria nyingine nchini zinazofanyiwa marekebisho
kwa dharura na nyingine kutungwa kwa Dharura Kutokana na uhitaji uliopo basi
wameomba Mh Rais ifanyike hivyo kwenye sheria hiyo ili kuwapatia haki wajane
waliowengi ambao wanakosa haki zao nchini.
Jana katika siku ya
maadhimisho ya Haki nchini Tanzania Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kuwa ni
Mjane Kutokea tanga alijitokeza mbele ya Rais Magufuli na
kufikisha kilio chake cha kudhulumiwa haki zake kutokana na kufariki kwa mume
wake ambapo baada ya maelezo hayo Mh Rais aliagiza swala hilo kushughulikiwa mara
moja na mwanamke huyo kupewa haki yake kisheria
No comments:
Post a Comment