Picha ya Pili na ya tatu zikimuonyesha Mwenyekiti wa Madereva wa Madereva wa Pikipiki Mkoa wa Dar es salaam Bwana Michael Massawe ambaye katika shughuli Hiyo alimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda. Ambapo akizungumza kwa Niaba yake amesema kuwa Mkoa wa Dar es salaam umejipanga kuhakikisha kuwa unawapa uwezo mkubwa madereva wa pikipiki ili waweze kufanya kazi zao kwa ustadi zaidi na kuepuka ajali na majanga ambayo yanaweza kuzuilika kwa urahisi,Amesema kuwa mafunzo kama hayo ambayo yamehitimishwa leo Katika kata ya Ndugumbi ni Mpango wa Serikali kupitia Trafic kikosi cha usalama Barabarani kuhakikisha kuwa madereva wanapatiwa elimu na kuwa na leseni zinazowafanya kuendesha Vyombo Hivyo bila madhara yoyote |
Diwani wa kata ya Ndugumbi Mh Thadei Massawe akizungumza na madereva hao 27 waliohitimu mafunzo hayo ambapo amewata kuhakikisha kuwa wanazingatia kile ambacho wamejifunza kwa siku hizo kumi huku akisisitiza kuwa endapo watafwata waliyofundishwa ana uhakika kuwa kutakuwa na kupungua kwa Ajali za bodaboda na matatizo ya ujambazi wa piki piki katika kata yake |
Baadhi ya Madereva waliohitimu mafunzo hayo leo Jijini Dar es salaam katika kata ya Ndgumbi |
No comments:
Post a Comment