Monday, February 20, 2017

FAUSTIN SUNGURA:MBATIA AJIMILIKISHA MALI ZA CHAMA


Faustin Sungura 

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi  JAMES  MBATIA pamoja na Katibu mkuu wa chama hicho MARTINI DANDA wamepewa siku tatu kujiuzulu ndani chama hicho kwa madai ya kujimilikisha mali za chama.

            Hayo yameelezwa na aliyekuwa mmoja wa waanzilishi na waasisi wa chama hicho baada ya madai kuwa mwenyekiti wa chama hicho JAMES MBATIA kujimilikisha shamba la hekhari 56 lilipo Kiromo,Bagamoyo Mkoani pwani pamoja na nyumba 2 zilizopo Bunju B ambazo zote ni mali ya chama hicho.

            Akizungumza na wahandishi wa habari jijini Dar es salaam muanzilishi wa chama hicho FAUSTIN SUNGURA amesema mali hizo zote walizinunua mwaka 2002 kama moja ya mali za chama kwa makubaliano maalum.

            Aidha SUNGURA amesema kuwa endapo hawatajiuzulu ndani ya siku tatu atafungua kesi  ya jinai mahakamani kama mwendesha mashtaka wa kujitegemea chini  ya sheria kifungu namba 99 cha makosa ya jinai.


            Hata hivyo amewaomba wanachama na wapenda haki na bila kujali itikadi wamuunge mkono kwa hali na mali katika harakati za kurudisha hadhi ya NCCR-mageuzi kwa kumuondoa mwenyekiti wa chama hicho.

No comments: