Wakati sakata la Madawa
ya kulevya nchini Tanzania likiendelea kushika vichwa vya habari katika
magazeti na Vyombo mbalimbali nchini Huku vigogo kadhaa wakiendelea kufanyiwa
uchunguzi juu ya Tuhuma hizo hatimaye Naye mwenyekiti wa Jukwaa la katiba
nchini Tanzania JUKATA Bwana Deus Kibamba ameibuka na kukosoa Vikali hatua
zinazochukuliwa na Viongozi wa serikali juu ya watuhumiwa wa madawa hayo.
Akizungumza na wanahabari
Juu ya kukwama kwa mchakato wa katiba mpya nchini na Jinsi ya kuuanzisha Upya
Deus amesema kuwa hatua ya kutaja majina ya viongozi na watu wenye heshima katika
jamii bila kuwa na ushahidi wa moja kwa moja na kabla vyombo husika vya
kitaalam havijadhibitisha kuhusika kwao ni mwendelezo wa kuwaficha wahusika
halisi wa madawa ya kulevya nchini na pia hatua hiyo inaendelea kupoteza
ushahidi halisi wa wahusika.
Ameongeza kuwa kumwita
mtu aje Kituo cha polisi kwa ajili ya kumfanyia mahojiano hawezi kuacha
kusafisha nyumba yake hata kama anahusika atajiandaa kwa kuhakikisha kuwa
nyumba inakuwa safi,huku akihoji mamlaka halali za kushughulika na madawa ya
kulevya nchini ziko wapi kwa kuwa kazi hiyo sasa inafanywa na watu ambao
hawakupewa mamlaka ya kufanya hivyo.
KUHUSU RAIS KUKUBALI
KUKOSOLEWA
Katika hatua nyingine
JUKATA pamoja na kulaani watu wanaotumia lugha za matusi kuwakosoa viongozi
wakuu wa nchi lakini hatua ya kuwakamata na kuwaweka ndani watu kwa makosa ya
kukosoa kwa lugha nzuri bila matusi ni kinyume cha katiba ya Tanzania huku
wakisisitiza kuwa hakuna kiongozi bora duniani asiyekubali kusikia mawazo ya
kukosolewa kutoka kwa wananchi wake.
Kibamba amesema kuwa
uvumilivu wa kisiasa unahitajika sana katika nchi kipindi hichi ambacho nchi inaongozwa na serikali mpya kwa
kuwa kumekuwa na matukio ambayo yanatisha ikiwemo watu kupotea bila kujulikana
walipo,na wengine kukutwa wakiwa wamefariki katika viroba na serikali kushindwa
kutoa maelezo yaliyokamilika kuhusu matukio hayo.
Moja kati ya mambo
ambayo ameyataja kuwa wameanza nayo katika kufufua mchakato huo ni pamoja na
kufanya mkutano mkuu wa katiba ambao utafanyika kuanzia Tarehe 2 hadi 3 mwezi
wa Tatu ambao utawashirikisha wadau mbalimbali wa katika nchini, pamoja na uzinduzi
wa Filamu mpya ya Dakika 20 itakayokuwa inaonyesha mchakato mzima wa katiba
mpya.
Katika hatua nyingine
JUKATA wametuma wito wa kufanya mazungumzo na Rais Wa Jamhuri Ya muungano wa Tanzania
Mh Dr John Pombe Magufuli kwa ajili ya kujadili naye maswala mbalimbali
yanayohusu Katiba mpya nchini pamoja na kumshauri Mambo kadhaa ya kupata katiba
Mpya.
No comments:
Post a Comment