Saturday, February 25, 2017

TIGO YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO KWA KITUO CHA AMANI MKOANI KILIMANJARO

Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata akitoa maelezo ya msaada wa vifaa vya michezo mbalimbali pamoja na vifaa vya Kilimarathon, vifaa hivyo vimetolewa kwa Kituo cha watoto cha Amani Children's Home cha mjini Moshi, Kilimanjaro, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Meindert Schaap.

 Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata (kulia) akimkabidhi jezi Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha watoto cha Amani Children's Home cha mjini Moshi, Kilimanjaro, Meindert Schaap ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya michezo uliotolewa na Tigo kwa ajili ya kituo hicho.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha watoto cha Amani Children's Home cha mjini Moshi, Kilimanjaro, Meindert Schaap akitoa shukrani kwa mtandao wa simu za mkononi wa Tigo baada ya kupokea msaada wa vifaa vya michezo mbalimbali vikiwemo vya Kilimarathon. Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata​

Watoto cha Amani Children's Home cha mjini Moshi, Kilimanjaro pamoja na  wafanyakazi wa Tigo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mtandao huo kukabidhi vifaa vya michezo.

Mtoto anayelelewa na  Amani Children's Home cha mjini Moshi, Kilimanjaro, Joyce Nganda akitoa neno la shukrani kwa waandishi wa habari baada ya kituo hicho kupokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka Tigo.

No comments: