Tuesday, February 21, 2017

USAJILI WA TIGO KILI HALF MARATHON WAENDELEA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Edger Damian akijisajili kwa njia ya Tigopesa kwa ajili ya mashindano ya Kili Marathon yatakayofanyika Kilimanjaro hivi karibuni. Usajili huo ulifanyika mwishoni mwa wiki.

Msajili wa Kili marathon wa Tigo, Neema Misaji akimpa maelekezo ya kulipa kwa njia ya tigo pesa, mkazi wa Dar es Salaam, Iyan Balegele aliyekuwa akilipia kupitia huduma hiyo mwishoni mwa wiki.

Wananchi mbalimbali wakijisajiri ili kupata tiketi za Kilimarathon kwenye banda la Tigo katika viwanja vya Mlimani city mwishoni mwa wiki.

Wakazi wa Dar es Salaam, Eden Mbunde na Sheila Kombe wakimsubiri Msajili wa Tigo, Viola Mboya aliyekuwa akimalizia usajili wao kabla ya kuwakabidhi tiketi zao mwishoni mwa wiki.

No comments: