Friday, March 31, 2017

HIVI UNAJUA KWAMBA SIMU YAKO INAWEZA KUKUPUNGUZIA UFANISI KAZINI?




Na Jumia Travel Tanzania



Inawezekana wewe ni miongoni wa watu wasioweza kustahimili kukaa mbali na simu hata kwa dakika moja. Ni suala gumu sana kwa wengi wetu kuweza kuitelekeza simu na kufanya shughuli nyingine kama vile tukiwa ofisini. Lakini je ushawahi kujiuliza kuna madhara gani kwa kuiendekeza tabia hiyo?  

Mahakama Kenya Imeizuia Serikali Kuajiri Madaktari Kutoka Tanzania


KENYA: Mahakama imeizuia Serikali kuajiri Madaktari kutoka Tanzania kwa sababu ndani ya nchi hiyo kuna Madaktari 1,400 wasioajiriwa.

Mpaka sasa takribani watanzania 400 wenye taaluma ya Utabibu wameomba kazi hiyo.

Rais Magufuli alikubali ombi la kupeleka Madaktari 500 ili kupunguza uhaba wa Madaktari nchini Kenya kutokana na mgomo unaoendelea nchini humo.

DR SLAA AANZA KUICHOKONOA SIASA YA TANZANIA,AZUNGUMZIA UONGOZI WA RAIS MAGUFULI


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dkt Willbrod Slaa alipozungumzia utendaji kazi wa Rais Magufuli amesema kuwa watu waelewe hakuna nchi hata moja ambayo kiongozi atakubalika na watu wote kwa asilimia 100.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania akiwa nchini Canada Alhamisi hii, Dk. Slaa ambaye amemaliza masomo yake na baada ya kufanya tafakari atarejea nchini wakati wowote.

Dkt Slaa alisema wako watu ambao maslahi yao yataguswa kwa namna moja au nyingine hivyo lazima watapiga kelele.

“Hatua zote zimechukuliwa,zinapaswa kuwa endelevu. Kwa bahati mbaya mchwa wengine waliopenya mpaka ndani ya Ikulu na Serikali na huwezi kufagia Serikali nzima kwa siku mmoja. Kwa jinsi Rais ambavyo hayumbi na wala hayumbishwi, nina hakika atafikia malengo na kurudisha Taifa kwenye misingi ya tunu za Taifa ya uwazi, ukweli, uadilifu, kuheshimiana na kuthaminiana na hasa kujali utu,” alisema.

“Hii ndiyo hali ambayo Rais Magufuli kila siku anaiita ‘Transition’ (kipindi cha mpito). Tutafika tu, tunatakiwa kuwa wavumilivu na wenye uzalendo wa kweli ana nia njema ya kufikisha Taifa mahali pazuri. Hii inahitaji kuweka pembeni maslahi yetu binafsi kama mtu mmoja mmoja, viongozi wa Serikali au hata wa kisiasa.”

CHADEMA YAPATA MSIBA WA UBUNGE WAKE


Thursday, March 30, 2017

AZAM, NDANDA KOMBE LA SHIRIKISHO LA ASFC 2016/2017

 
Robo Fainali ya tatu ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup 2016/2017), kati ya Azam FC na Ndanda FC itafanyika Aprili 5, 2017 saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, imefahamika.

Kadhalika, Robo Fainali ya nne ya mwisho ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup 2016/2017), kati ya Young Africans na Tanzania Prisons FC itafanyika Aprili 22, 2017 saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Washindi wa kila mchezo watasonga mbele kwenda Raundi ya Nane ambayo ni Nusu Fainali. Tayari klabu za Mbao na Simba zilitangulia hatua hiyo ya Nusu Fainali.

Mbao FC ya Mwanza nayo imetangulia hatua ya Nusu Fainali baada ya kuilaza Kagera Sugar mabao 2-1 katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera Machi 18, mwaka huu.

Kwa upande wake, Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imepita baada ya kuishinda Madini FC ya Arusha kwa bao 1-0 katika mchezo wa Robo Fainali ya pili uliofanyika Machi 19, 2017 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.


……………………………………………………………………………………………
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

WANAWAKE WASHIKA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI MASOKONI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Soko la Gezaulole lililopo Kiwalani Bomu bomu, Muhidin Waziri 'Ndolanga' akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu changamoto iliyokuwepo katika soko hilo juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo hivi sasa vimedhibitiwa baada ya kupata mafunzo kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG). Kulia ni Mwezeshaji wa Kisheria wa soko hilo.

Mtangazaji Clouds Afukuzwa Kazi kwa Kumtaja Makonda Kwenye kipindi,TEF wapongeza Hatua Hiyo

Taarifa Kuhusu Kutoandika Habari za RC Makonda

Bodi ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) imekutana jijini Dar es Salaam leo Machi 30, 2017. Pamoja na mambo mengine imejadili mwenendo wa vyombo vya habari ndani ya wiki moja tangu tulipotoa msimamo wa kutotangaza habari za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Bodi imepitia habari za Mkuu wa Mkoa zilizochapishwa tangu ulipotolewa msimamo wa kumfungia.

Bodi inapenda kawapongeza wahariri wote waliotekeleza kwa usahihi msimamo wa kutochapisha habari za Mkuu wa Mkoa kwa wiki nzima.

Bodi inapenda kusisitiza kuwa wahariri katika vyombo vya habari; magazeti, radio na televisheni waendelee na msimamo wa kususia habari za Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, hadi atakapotimiza takwa la kuomba radhi kwa tukio la kuvamia kituo cha Clouds.

Bodi inatoa wito kwa viongozi wa mitandao ya kijamii kuunga msimamo huu.

Bodi inapenda kufafanua kuwa Mhe. Makonda amewekewa vikwazo Maalum (Smart Sanction) kwa mikutano atakayoiandaa au matukio atakayoyaongoza habari zake hatutazichapisha.

Bodi inakipongeza Kituo cha Clouds kwa kumsimamisha kazi mtangazaji aliyekiuka msimamo wa kutotangaza habari za Makonda.

Bodi pia imewasiliana na Uongozi wa UTPC na kukubaliana kwamba msimamo huu uendelee.

Theophil Makunga,
Mwenyekiti TEF

Imetolewa Leo,
Machi 30, 2017

MBUNGE LIJUALIKALI WA CHADEMA AACHIWA HURU

IMG_20170330_104142Mbunge wa Kilombero Lijualikali yuko huru baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar kutengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Kilombero

Mbowe Azua Jipya..Adai Bajeti ya Serikali Haitekeleziki..Wajiandaa Kuipinga Bungeni

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema wataipinga bungeni bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2017/18 kwani haina msaada wowote kwa wananchi wa hali ya chini na wanaamini fedha hizo hazitapatikana kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mbowe amesisitiza mwaka jana wabunge wa kambi ya upinzani walieleza wazi kuwa bajeti ya mwaka huu isingetekelezeka na ndio kilichotokea kwani mpaka sasa asilimia 34 pekee ya pesa zote za maendeleo ndizo zimetolewa.