Friday, March 24, 2017

COCA-COLA YAZIDI KUHAMASISHA WANAFUNZI KUTAMBUA NA KUKUZA VIPAJI VYAO

Wafanyakazi wa Coca-Cola wakiwagawia wanafunzia wa Shule ya Sekondari ya Olorieni Vinywaji vya Coca-Cola katika eneo la shule hiyo.
Mwanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni akionyesha kipaji cha kucheza na Baiskeli kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule mbalimbali.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakionyesha kipaji cha kucheza na baiskeli kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule mbalimbali.

Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakicheza wimbo wa Kijuso (jukwaani) huku wenzao wakiwatazama kwenye promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule mbalimbali jijini Arusha.
Wanafunzi wa wawili wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakionyesha kipaji cha kucheza muziki kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola katika shule mbalimbali.
Mwongozaji wa Promosheni (Supervisor) Onesmo Swila Akimkabidhi zawadi ya mipira ya miguu mwalimu wa michezo wa shule ya Sekondari ya Olorieni katika promosheni yao ya Onja msisimko na Coca-ola inayoendeshwa katika shule mbalimbali jijjini Arusha.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakionyesha kipaji cha kuimba kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule mbalimbali.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakicheza wimbo wa Kijuso (jukwaani) huku wenzao wakiwatazama kwenye promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule mbalimbali jijini Arusha.
Wanafunzi  wa  Shule ya sekondari ya Olorieni wakigongeana sheazi mara baada ya kugawiwa vinywaji   kwenye  promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko  katika shule mbalimbali jijini Arusha.  (Picha na Ferdinand Shayo). --- Kampuni ya Bonite Bottlers Kupitia kinywaji chake cha Coca-Cola imezidi kuhamsisha wanafunzi kutambua na kukuza vipaji vyao kupitia Promotioni ya Onja Msisimko na Coca-Cola wanayoiendesha katika shule mbalimbali jijini Arusha. Cocacola imefanya hayo katika shule Sekondari ya Olorieni jijini Arusha ambapo baadhi ya wanafunzi walipata Fursa ya kuonyesha vipaji vyao ikiwemo kucheza na baiskeli katika jukwaa, kucheza muziki pamoja na kuimba. Msimamizi wa promosheni hiyo Onesmo Swila amewataka wanafunzi katika shule hizo wanazotembelea ikiwemo Sekondari ya Olorieni ambayo wameitembelea, kuendeleza vipaji vyao kwa kila fursa wanayopata kwa kuwa kipaji ni hazina. “wanafunzi acheni kuficha vipaji vyenu, vionyesheni, ili mpate fursa ya kuvikuza, sisi Coca-Cola tumeamua kuwahamasisha kwa lengo kuwatia moyo ili mfikie malengo yenu.” Alisema Onesmo Aidha licha ya kuwashukuru walimu wa shule hiyo kwa kuwakubalia kutembelea shule hiyo na kuwagawia wanafunzi zawadi ikiwemo ya kinywaji cha Coca-Cola, amesema ziara hiyo wataendelea nayo katika shule mbalimbali jiji Arusha ili kuwaonjesha wanafunzi Msisimko wa Coca-Cola. Mwalimu wa Michezo katika Shule ya Sekondari ya Olorieni, Haroon Maluli akipokea zawadi ya Mipira kutoka Coca-Cola, Ameshukuru kwa zawadi hiyo huku akiwasihi wanafunzi kutoficha vipaji vyao, bali wavionyeshe kwa kila fursa inayopatikana ili kuvikuza zaidi. “Tunashukuru kwa zawadi ya mipira, ila nawasihi wanafunzi kutumia fursa kama hii iliyoletwa na Coca-Cola kuonyesha vipawa vyenu, kwani hata sisi tulivyokuwa tunasoma hatukuvificha ndio maana tupo hapa” alisema Mwalimu Haroon.

No comments: