Covenant ni benki inayowajali wananchi wa hali ya chini na idara binafsi. Leo kikundi hiki cha farasi kimeweza kutimiza mwaka mmoja. Kikiwa
ni kikundi kilichoweka fedha zake katika benki hiyo na kuweza kupewa mwongozo
jinsi ya kunufaika na huduma za benki hiyo. Wanachama wa kikundi hiko walianza
wakiwa 20 na na kwa sasa wapo 40 na bado kuna wengine wanaomba kujiunga.
Grace Boniphace Luwiku Mwenyekiti wa kikundi hiko alisema kuwa wanafurahia
mafanikio ya mwaka mmoja wakiwa ndani ya Covenant kwa kuwa waliweza kutimiza
malengo yao
waliyo ya kusudia. walihitaji kuwa na biashara ya pamoja waliweza kufanikiwa na walihitaji kila mwanachama awe na biashara
yake waliweza pia na waliona kitu muhimu ni afya waliweza kukatiwa bima ya
afya ya AAR.
Na kwa leo wanaweza kufurahia mafanikio waliyoyapata ndani ya
mwaka mmoja.
MKURUGENZI MTENDAJI WA COVENANT BENKI SABETHA MWAMBENJA AKIONGEA NA VYOMBO VYA HABARI KWA KUKIPONGEZA KIKUNDI CHA FARASI KUTIMIZA MWAKA MMOJA. |
Mkurugenzi mtendaji wa Covenant benki Sabetha Mwambenja aliweza
kuwapongeza kwa kutimiza mwaka mmoja. Na kuweza kutimiza sehemu kubwa ya malengo yao ikiwa hivi karibuni wanafungua mgahawa wa chakula na vitu vingine mbalimbali. lakini pia wao kama
benki waliweza kuwasaidia kununua hisa za
kampuni ya Vodacom. Na kitu kingine aliweza kuwasifu kwamba wao
hawavunji tofauti na vikundi vingine wanaweka pesa zikiwa nyingi wanavunja na
kugawana. lakini hawa wako tofauti kwa kuwa wao wanakopeshana ndani ya kikundi
na mtu anarudisha kwa riba na baadae pesa inayopatikana wanagawana kama faida. Hii inaweza kuwasaidia kwa benki kuweza kuwaamini
na kuwapa huduma nyingine kubwa ikiwemo mikopo mikubwa ya kujiendesha wenyewe ndani ya kikundi.
MWENYEKITI WA KIKUNDI CHA FARASI AKIELEZEA MAFANIKIO WALIYO YAPATA NDANI YA MWAKA MMOJA WAKIWA CHINI YA COVENANT BENKI. |
BAADHI WANACHAMA WA KIKUNDI CHA FARASI GROUP WAKIWA KATIKA KUSHEREHEKEA WALICHOKIVUNA NDANI YA MWAKA MMOJA WA KIKUNDI HIKO. NA MWANDISHI WETU VICENT MACHA. |
No comments:
Post a Comment