Monday, March 20, 2017

DHEHEBU LA SHIA LIMEADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA KWA BI. FATMA A.S)

Kila ifikapo tarehe 20 ya mwezi machi waislamu kote duniani wana adhimisha maadhimisho ya mazazi ya Bi. Fatma A.S).  Akiongea na vyombo vya habari kiongozi shekh mkuu wa dhehebu la Shia Tanzania Shekh Hemedi Jalala alisema kuwa inakumbukwa siku hiyo kuwa ni muhimu kwa kuwa ni siku aliyezaliwa mwanamke huyo ambae ni uzao wa Mtume Mohamad na mchango wake wa dhati katika jamii na kwa dini ya Kiislam.
Sheikh Hemed Jalala akielezea ukubwa wa siku hii kwa dini yao

Alisema kuwa mchango wa Bi Fatma unatambulika duniani kote na yeye aliweza kuwa mfano mzuri kwa wanawake wa kiislamu kuondoa fikra potofu zinazosema kuwa uislam unawanyima wanawake haki zao. Alisema kuwa hii si kweli kwa maana uislamu ni dini ya haki na inaweka usawa kwa pande zote kwa wanawake na wanaume na pia kila jambo zuri analolifanya mwanaume jua nyuma yake kuna mchango wa mwanamke. Mfano mtume mohamad aliweza kufanikisha kazi ya mungu kwa kuwa nyuma yake alikuwepo Bi Khadija katika kumtia moyo na kumsaidia baadhi ya mambo.
Sheikh Hamad Jalala kulia akiwa na kiongozi mkuu sheikh Mohamad Abdu
Alisema katika nafasi ya uongozi mwanamke anaruhusiwa kugombea nafasi yeyote hata ni juu hata kuajiri na pia kuajiriwa. Pia hata kusimama mbele na kufundisha dini imempa mamalaka hayo. lakini pia mwanamke ananafasi ya kupata urithi ikiwa ni kwa baba yake mama kaka na hata mume wake. Na pia katika kuachana sio lazima mwanaume hata mwanamke anaweza kumuacha mwanaume kama hakumpenda.

Na mwisho aliweza kuwashukuru wananawke wote na kuwatia moyo kwa kuwa wao ndio wanaofanya kazi kubwa ya kuzalisha hao wanaume wanaoheshimiwa leo. Kuweza kuwaomba kuadhimisha siki hiyo kwa furaha kwa kuwa ni siku kubwa kwao na kwa dunia nzima.

No comments: