Waziri wa Mambo ya Katiba na
Sheria, Mhe. Dkt Harrisson Mwakyembe amesema Serikali haiwezi kuona Chama cha
Wanasheria Tanganyika (TLS) kinajiingiza katika siasa na kama TLS wanataka
hivyo, basi Serikali haitasita kuifuta Sheria ya TLS Sura ya 307 iliyoanzisha
chama hicho cha Wanasheria.
Amesema kuwaingiza wanachama ambao
wana nasaba za siasa au viongozi wa vyama vya siasa ndani ya TLS ni kuruhusu
mgongano wa maslahi na yeye kama mwanasheria hawezi kulikubali jambo hilo. DKt
Mwakyembe alikuwa akizungumza hayo na ugeni wa Chama cha Wanasheria Tanganyika
(TLS) uliokuja kumtembelea Ofisini kwake mjini Dodoma ukiongozwa na Rais wao
Bw. John Seka
“Kama Wizara hatujui mwelekeo wa
TLS kwa sasa, hatuwezi kuiacha TLS ikijiingiza katika siasa halafu tukawaangalia
tu. Hatuna nia ya kuitawala TLS, ila tunawajibika kuwasimamia kwa kuwa Sheria
yenu iko chini yetu, mkiharibu kwa lolote Wizara ndio yenye wajibu wa kuwatolea
maelezo, katika hilo mnalotaka kulifanya sasa kuna mgongano wa maslahi, je nyinyi
kama wanasheria hamkuliona au hamlioni?, alisema Mhe Mwakyembe.
Alisema Serikali haina shida na
wanachama wa TLS kuwa wanachama wa vyama vya siasa ila ni lazima wafahamu kwamba
viongozi wanaowachagua ambao ndio watakaobeba sura ya TLS na mwelekeo mzima wa
chama kama wanataaluma hawapaswi kuwa na nasaba za kisiasa ili kuepusha
mgongano wa maslahi unapoweza kujitokeza.
“Serikali haina shida na
wanachama wa TLS kuwa wanachama wa vyama vya siasa ila tatizo linakuja pale mnapotaka
kuchagua viongozi ambao tayari wanazo kofia mbalimbali za uongozi ndani ya vyama
vya siasa, hao ndio watakaobeba sura na mtazamo au mwelekeo wenu hapo hatuwezi
kukubali kwa kuwa watatenganishaje uongozi wao katika chama husika na uongozi
wao ndani ya TLS, huo sasa ndio mgongano wa maslahi alisema Dkt. Mwakyembe na
kuongeza kuwa ndio maana mwanasheria yoyote akiingia katika utumishi wa umma uwakili
wa kujitegemea anauweka pembeni ili kuepuka mgongano wa maslahi.”
Alisema TLS sasa imekuwa na
haihitaji muangalizi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma nchi ilipopata uhuru, kwani
ina wasomi wengi na vijana wengi wamekuwa wanachama pia na kwa hiyo ni bora
tuifute hii Sheria yenu na tuwape mwanya mkajisajili kama NGO ambako kiongozi
yeyote wa chama cha siasa anaweza kuwa kiongozi wao.
Amewataka wafahamu kuwa dhamira
ya Serikali ni njema huku ikizingatiwa kwamba Sheria kama zilizvyo taaluma
nyingine nchini bado zinahitaji uangalizi hasa ukizingatia uingiaji wa nchi
katika utengamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akizungumza katika kikao hicho
Katibu Mkuu wa Wizara Prof. Sifuni Mchome alisema kila taaluma ina namna ya
uangalizi wake. alisema kama wanasheria lazima kuhakikisha hatutoi vipaumbele
kwa siasa kama zilivyo fani nyingine nchini. Alitaka wajiulize kama kweli hawauoni
mgongano wa maslahi huku wakizingatia kuwa wanapaswa kuhudumia jamii ya
watanzania bila ya kuwabagua.
“Kama wanasheria lazima
tuhakikishe hatutoi vipaumbele kwa siasa kama zilivyo fani nyingine, jiulizeni
kama kweli hamlioni jmabo hilo kama ni kikwazo huku mkizingatia kuwa tunatakiwa
kuhudumia jamii bila ya kuwabagua sasa
tukijiingiza katika siasa tutaihudumiaje jamii husika? TLS kutojihusisha na
siasa ni miongoni mwa kanuni za kutuimarisha kama wanataaluma,”alisema Prof
Mchome
Alisema Wizara ipo kuiangalia TLS,
na ndicho ilichofanya, imewastua jamani mnaenda wapi? tunataka muende katika
mstari sahihi, nawataka mjiulize hivi kweli kamati ya uchaguzi haijaona kama
kuna mgongano wamaslahi hapo?
“Tupo hapa kuwangaalia, na ndicho
tulichofanya, tumewashtua jamani mnanenda wapi? Hatuna nia mbaya ila tunawataka
muwe katika mstari, hivi kweli kamati ya uchaguzi haijaona kama kuna mgongano
wa maslahi hapo?
Alisema Serikali haitasita
kuchukua hatua ya kuifuta Sheria ya TLS kama chama hicho kitaendelea na msimamo
wa kujihusisha na masuala ya siasa au kiuharakati chama hicho katika siasa na hawana budi zaidi
ya kuangalia namna wanavyoweza kujikwamua katika hilo.
Kama hamuwezi kuendeleza misingi
ya kitaaluma ya kutojihusisha na siasa au vyama vya siasa basi serikali
haitakuwa na namna zaidi ya kuifuta sheria ya TLS na TLS ya sasa itabidi
ikajisajili kama NGO ili iendeleze harakati zake na Serikali itaunda sheria
nyingine itakayoanzisha chombo kitakachosimamia misingi ya kitaaluma.
Naye Rais wa TLS bw. John Seka
akizungumza katika kikao hicho alisema ameelewa maoni ya Serikali na kwamba
kuonekama kwa TLS kama inajiingiza katika siasa kunatokana na wanachama ambao
ni viongozi au wanachama katika vyama vya siasa ambao kwa sasa wanataka uongozi
wa chama hicho.
Ameiahidi serikali kuwa TLS
itaendelea kuzingatia kanuni na miongozo ya kuanzishwa kwake ambapo pia haina
mpango wakuwa chama cha siasa au chama cha kiharakati na hivyo kuiomba Serikali
kuifanyia marekesbisho Sheria yake ili iweze kukabili changamoto inazokabilian nazo
kama ilivyotokea sasa ambapo mwanachama ni kiongozi wa chama cha siasa na hivyo
kuwa na haki ya kuomba uongozi wa TLS
Amesema anaiomba wizara na
watendaji wake kuendelea katika mazunguimzo na TLS ili kuweza kuhakikisha
inatekeleza na kufikia malengo yote ya kuanzishwa kwake huku akiahidi kuwa siku
zote TLS haitogwanyika, itasimamia na kuongoza wanachama wake ipasavyo na
kuhakikisha misingi na maadili ya taaluma ya sheria inazingatiwa ili TLS
iendelee kubaki kama ilivyo sasa na kutokupendelea upande wowote.
No comments:
Post a Comment