Deus Kibamba Mwenyekiti wa Jukwaa La katiba Tanzania |
Jukwaa
la katiba nchini Tanzania leo limezindua mkutano wake utakaodumu kwa siku mbili
ukiwa na lengo la kuitaka serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kutoa
mustakabadhi wa katiba mpya baada ya kudai kuwa mchakato ulianzishwa na Rais
mstaafu wa awamu ya nne Mh. Jakaya Mrisho Kikwete na kuhitaji serikali ya awamu
ya tano kuweza kumalizia mchakato huo.
Mkutano huo uliyoudhuriwa na watu mbalimbali kutoka vyama
mbalimbali ya siasa nchini na asasi zisizo za kiselikali na Maprofesa pamoja na
waandishi wa habari lengo ni kuweza kupaza sauti kwa pamoja ili kuweza
kuhamasisha wahusika wa tatizo hilo.
Pia aliongezea kwa kusema vyama vya siasa vinatakiwa kuwa mstari
wa mbele kwenye hili kwa maana ipo kwenye ilani ya vyama vyao iliwemo chama
tawala cha CCM kilisema kuwa kikishinda kitahakikisha kinaipatia taifa katiba
mpya vivyo hivyo na chama kinachounda umoja wa UKAWA pamoja na ACT
wazalendo.Ila kwa kuwa CCM ndio kimeshinda basi kinatakiwa kutimza azma yake ya
kuwapatia wananchi katiba mpya kwa kuwa ni haki yao ya msingi.
Aidha Jukata wanasikitishwa na kwa kauli ya Rais aliyosema kuwa
wakati anaomba kura hakusema kuwa atabadilisha katiba iliyopo kwa kauli hiyo
jukata wameomba kujua kwamba wakati
anazindua bunge aliposema kuwa najua kuna kiporo cha katiba alikuwa akiongelea
kisiasa tu au alikuwa akimaanisha kweli.
Katika Hatua nyingine Jukata wamepongeza jitihada za mzee Warioba kwa kuwasilisha
katiba yenye maoni ya wananchi na sio katiba iliyopendekezwa kwa kuwa katiba
iliyopendekezwa ilikuwa na mapungufu mengi na kingine katiba hiyo ilikuwa
ikiwapa nguvu kubwa chama tawala.
No comments:
Post a Comment