JUKATA WAHITIMISHA MKUTANO WAO WA KATIBA


Bw. Othumani Masoud Othuman aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar akitoa maoni yake katika mkutano huo
 Na Vicent Macha

Jukwaa la katiba nchini Tanzania JUKATA jana limefikiia kilele cha mkutano wake mkuu wa katiba kwa kuweza kuwaalika wadau mbalimbali akiwemo Bw. Othumani Masoud Othuman akielezea kero na changamoto zilizopo kwenye katiba kwa upande wa tanzania visiwani. 

Pamoja na prof. bertha o.koda yeye akielezea kuhusu mchango wa wanawake katika kukwamua mchakato wa katiba mpya ya tanzania bara mkutano huo uliodumu kwa muda wa siku mbili uliodumu kwa muda wa siku mbili uliweza kufanyika Land Mark Hotel jijini Dar es salaam.
Deus Kibamba Mwenyekiti wa Jukata akitoa mada
Bw. Othumani Masoud Othumani yeye alijikita zaidi kwenye muungano na kusema kuwa muungano huu haupo sawa kwa maana katiba inaibeba sana tanganyika kuliko zanziba akatolea mfano kwamba jambo linapokuwa ni la kuhusu zanzibar linakwenda kujadiliwa bungeni na wabunge wangi wakipinga basi linatupiliwa mbali kwa kuwa baraza la wawakilishi waliopo bungeni haliwezi kushindana na wabunge wa bara kwa kuwa wao ni wengi na watashinda tu.

Aidha aliongezea kitu kingine akisema kuwa mjadala wa kuwa zanziba ni nchi au la kwamba kwenye katiba kuna kifungu kinasema kuwa ni sehemu ya Tanzania lakini hakuweki wazi wazanzibar wanajiuliza au ni mkoa ndani ya Tanzania kwa kuwa halijawekwa wazi ni sehemu gani ya nchi hiyo.

Lakini pia wanasikitishwa kwa kuona Zanzibar inachukuliwa kama mtoto na bara kama mzazi kwa maana hata kesi zinatoka Zanzibar na kuja kusikilizwa mahakama kuu ya bara. na hata ikitokea swala la kuitajika waziri wa Tanzania anatoka kwa Tanganyika kwa  nini wasipewe nafasi na kwao kwa kuwa ni watanzania wote na wapo kwa ajili ya muungano, lakini pia raisi Mkapa alipoingia madarakani mwaka 2000 alisema kero za muungano nitazimaliza ndani ya siku 60 lakini mpaka leo haikuwa ivyo wanajiuliza toka mwaka huo mpaka leo siku sitini bado hazijafika?

Prof.Bertha O. Koda alieleza makudi mbalimbali ya wanawake wanavyoweza kujitolea katika kujikwamua kotoka tulipo mpaka kuipata katiba mpya. na ameweza kupongeza makudi mbali mbali yaliyojitolea kuweza kuelimishana kuweza kuipigania katiba mpya ikiwemo TAMWA, TGNP na mengine mengi yanyotoa miongozo na kutoa maoni yao ili kuweza kupata usawa wa kijinsia katika nafasi mbalimbali. 

Prof Koda alisema inabidi kuipigania katiba ili maoni yao ya usawa yaweze kuwepo kwa maana mfumo wa uongozi hata kwenye uwaziri haukuweza kuwapa nafasi nyingi wanawake na hata pia kwa upande wa dini bado wanume wamekuwa wakichukua nafasi kubwa na wanawake wanakuwa chini yao hivyo wanahitaji kuondoa dhima ya mfumo dume.
Mwenyekiti wa Jukuta Bwa Deusi Kibamba aliweza kuhitimisha kwa kusema mkutano ulikuwa mzuri sana na hawakutarajia ungeibua mambo mengi kiasi kile na wanashukuru kwa wote walioudhuria kwa namna moja ua nyingne na wanaimani ujumbe utaweza kuwafikia wahusika kwa maana wao wanaamini kuwa raisi alijisahau na kwa njia hii ataweza kukumbuka na pia wanakusudia kufanya mkutano mkubwa wa pili endapo wataona bado sauti yao haijafika mahala husika.About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.