Wednesday, March 15, 2017

Kampuni ya Quality Group LTD yaelezea mipango mipya ya miradi yake nchini



Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Quality Group Limited, Bwana. Nicholas Ralph leo Machi 15.2017, amekutana na vyombo  vya habari na kuelezea mipango mbalimbali ya kampuni hiyo ikiwemo miradi yake inayoendeshwa karibu nchi nzima Tanzania Bara na Visiwani.

Akizungumza na vyombo mbalimbali  katika tukio lililofanyika majira ya Alasiri ya leo Machi 15, Mkurugenzi huyo ameweza kuweka bayana miradi yao hiyo pamoja na muelekeo wa kampuni katika kufikia malengo yake  huku akibainisha kuwa, wataendelea kufanya kwa kiwango cha hali ya juu ikiwemo kuwafikia wananchi kama sera ya makampuni hayo na ile ya Taifa huku wakiungana na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli  ya kupiga vita rushwa na kuifanya Tanzania ya Viwanda.

Akielezea muelekeo wa kampuni hiyo amebainisha kuwa watanzania wanaimani nao hivyo wataendelea kujikita zaidi kwenye miradi na kuwafikia watanzania sehemu mbalimbali kama dira yao ya kuiletea Tanzania maendeleo yaani 2016/2021 na ile ya mpaka 2025 
“Quality Group imeweza na inaendelea kushirikiana na makampuni yenye majina makubwa Duniani kwa kufanya nao kazi pamoja na uwakala kwa hapa Tanzania ikiwemo kampuni za GM, Hoda,Isuzu, Bridgestone pamoja na  Chevrolet  huku yakizalisha faida maradufu hii ni pamoja na kutoa ajira kwa watanzania” amesema Mkurugenzi huyo.

Aidha, akitaja baadhi ya miradi ambayo inasimamiwa na kampuni hiyo hapa nchini ni pamoja na mradi wa shamba la mpunga lililopo Mkoani Morogoro ambalo litakuwa likipanda mazao hayo sambamba na kununua kwa wakulima wadogowadogo ili kupata mchele.
Quality Group pia inasimamia miradi Visiwani Zanzibar ikiwemo ule wa Stone Town Village huku pia mirad mingine ni ule wa  Matrekta ambao ni wa Sonalika.
Kampuni hiyo kwa hapa nchini ni ya miaka mingi zaidi ya miaka 30 huku ikiwa imeweza kuajili wafanyakazi zaidi ya 667,300 huku ikitengeneza zaidi ya  faida  Bilioni 348.6 huku wa miongoni mwa makampuni bora na yenye majina makubwa kwa kujijengea heshima ndani na nje ya nchi.

No comments: