Tuesday, March 21, 2017

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHA MSHINIKIZA RAIS KUMTUMBUA MAKONDA

Kituo cha sheria na haki za binadamu leo kimtoa tamko juuu ya sakata linaloendelea la Mh. Paul Makonda la kuvamia kituo cha televisheni cha clouds tv.
Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) BI. Helen kijo Bisimba akitoa ufafanuzi wa kinachoendelea nchini.
Kituo hicho kime laani vikali hali hiyo kwa maana kwa kufanya hivyo ni kuingilia uhuru wa vyombo vya habari na ni kukiuka haki za binadamu na utawala bora. Inaeleweka kuwa kunasheria zinazoweza kusababisha kiongozi mwenye dhamana kuweza kufungia au kutoa onyo kwa chombo cha habari endapo kitafanya kosa. 

Lakini hakuna sheria inayosema kiongozi kushinikiza chombo cha habari kufanya kitu ambacho ni matakwa yake na kwa maslahi yake binafsi na siyo kwa maslahi ya taifa.
Pia imeelezwa kuwa vitendo kama hivyo vinatakiwa kukemewa vikali hapa nchini kwa kuwa ni matumizi mabaya ya uongozi. Na kwa hili selikali kupitia kiongozi mwenye dhamana hiyo  ilitakiwa kuchukua hatua kwa kumuwajibisha mkuu wa mkoa huyo.
Baadhi ya wanahabari wakisikiliza tamko toka kwa kituo cha haki za binaadamu.

Bi Helen Kijo Bisimba alisema inafahamika kuwa kuna sheria kandamizi juu ya vyombo vya habari na hata muda mwingine hutishia kufungia vyombo hivyo. lakini hakuna sheria inayomtaka kiongozi yeyote kutumia chombo cha habari kwa maslahi yake binafsi.

Walisema kuwa wanampongeza Raisi kwa kauli yake mbiu ya “HAPA KAZI TU” kwa kuwa inawapa motisha wananchi wa kufanya kazi kwa bidii. Lakini walishangazwa na Raisi huyo baada ya kutoa onyo kwa Bw. Makonda kwa alichokifanya lakini matokeo yake ameweza kupongeza kwa kumwambia wewe piga kazi tu usisikilize maneno yao hii inaonyesha kuwa Raisi John Pombe Magufuli karidhika na kitendo iko.
waaandishi wa habari wakiwa kazini

Alimalizia kwa kusema wanavitaka vyombo vya habari kuweza kuungana na kutetea maslahi na uhuru wa habari kuacha kujiendesha vyenyewe kwa maslahi binafsi huku vikiachauweledi wa vyombo hivyo kuzidi kudidimia. Na watanzania kwa ujumla kuweza kukemea tabia kama hizi za wakina makonda. Na mwisho selikali inatakiwa kuchukua hatua za kinidhamu  na kijinai kumuwajibisha makonda kwa maana alichokifanya ni koasa la jinai chini ya kanuni za makosa za adhabu 2002.

No comments: